MAKUNDI YA WAISLAMU

waislamu wamegawanyika katika makundi makuu matatu: Kuna waislamu wanaamini na kusifu viongozi wao kupita kiasi (zaidi ya anavyostahili kusifiwa) na kuamini kila aina ya uzushi kuhusu viongozi wao bila kuwa na dalili. Wako waislamu wengine ambao wapo kati kwa kati, yaani wanamsifu kiongozi au viongozi wao kwa namna inayostahili na wapo waislamu ambao wanapinga na kukebehi kila jambo zuri la kiongozi au viongozi wao hata kama watapewa ushahidi wa wazi.
Kwa mfano Masufi wanasema kuwa kuna uwezekano wa sheikh Abdul-Qadir Jailan kuwepo Baghdad na wakati huo huo akawa Tanzania, na huenda akamponya mgonjwa huko Misri na kumuokoa mtu anayezama katika bahari ya Pasifiki. Basi huku ni kuvuka mipaka ya kumsifu mtu (ifrat).
Nao Mawahhabi kwa kuwapinga Masufi wakakanusha kila kitu mpaka wamesema kuwa, ni shirk kutawassal kwa Mtume (S.A.W) na hii ni kupuuza haki inayomstahiki Mtume (tafrit).
Lakini Shia ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya kitabu chake kitukufu, 'Namna hivyo, tumekufanyeni kuwa ni umati wa kati na kati ili muwe mashahidi juu ya watu' (2:143). Hivyo Shia humsifu mtu kwa stahiki yake na kama ni mwovu hueleza uovu wa mtu kwa kiwango kile kile alichokifanya.

Comments