MAMBO YALIYO MWANGAMIZA MUAWIYAH BIN ABU-SUFIAN

Abul-A'ala Al-Maududi, Mwenyezi Mungu amrehemu amesema katika kitabu chake kiitwacho, "Ukhalifa na lifetime" katika ukurasa wa 106 akimnukuu Al-Hasan Al-Basri aliposema, "Mambo manne alikuwa nayo Muawiyyah, lau angekuwa na jambo moja miongoni mwa hayo lingetosha kumuangamiza.
1) Kuchukua ukhalifa bila ya mashauriano ya Waislamu na hali wamo miongoni mwao waliobakia Masahaba na wenye nuru ya ubora.
2) Kumpa Ukhalifa baada yake mwanawe mlevi ambaye alikuwa akivaa hariri na kupiga magitaa.
3) Kumfanya Ibn Ziyad kuwa ni mwana wa baba yake na hali Mtume (s.a.w.) amesema "Mtoto ni wa kitanda na mzinifu mwanaume atapata jiwe."
4) Kumuua kwake Hujr na Jamaa za Hujr, basi ole wake kwa kumuua Hujr na jamaa zake Hujr (akakariri mara tatu).
Mwenyezi Mungu amrehemu Abu A'ala Al-Maududi, kwa kupasua ukweli, na lau angetaka angeongeza zaidi ya mambo haya manne yakawa mambo arobaini lakini aliona kwamba hayo yanatosheleza kumuangamiza Muawiyyah na watu wanaomfuatia katika imani na matendo yake potofu.
Ninawaomba Ahlul-Sunnah wal-Jamaa kukiri na kuwafahamisha wenzi wao kwamba, "Watu ambao hawaukubali Uimamu wa watu hawa (Muawiyya Yazid, Abubakr, Omar na Uthman) na wala hawawatawalishi, wao ni Waislamu wanaostahiki heshima na jambo hilo halina shaka, museme ya kwamba Mashia ni wenye kudhulumiwa siku zote kwani wao hawakuufuata na kuukubali Uimamu wa (bani Umayyah) mti uliolaaniwa ambao Mwenyezi Mungu ameupigia mfano ndani ya Qur'ani.
Mashia wanatekeleza amri ya Mtume (s.a.w.w) inayosema: "Nimekuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu, vitu ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtapotea baada yangu." Kama ambavyo zinashuhudia Sihah za Sunni ukiachilia mbali vitabu vya Kishia.
Badala ya kuwashukuru (Mashia) na kuwatanguliza na kuwaboresha juu ya wengine kwa kufuata kwao maamrisho ya Mtume (s.a.w.w.), tunawashutumu na kuwakufurisha na kujitenga nao, jambo hili siyo uadilifu wala haliingii akilini.

Comments