Amesema
Bukhari na Muslim na wengineo kuwa: Imepokewa kutoka kwa Azzuhry naye amepokea
kwa U'rwa bin Zubeir naye amepokea kwa Mwana Aisha (mkewe Mtume) kwamba:
Malaika Jibril (a.s) alikuja kwa Mtume (s.a.w.) naye akiwa katika pango la
Hiraa akamwambia: Soma, Mtume akajibu: Mimi sijui kusoma. Mtume anasema:
Malaika akanikaba kwa nguvu mpaka nikazidiwa kisha akaniambia: Soma, Mtume
akajibu: Mimi sijui kusoma. Kisha ndipo Malaika alipomsisitiza kwa nguvu
akisema:
"Soma
kwa jina la Mola wako, ambaye ameumba. Amemuumba mwanadamu kutokana na damu
iliyoganda. Soma na Mola wako ni Mtukufu kuliko wote". Qur'an, 96:1-3
Baada
ya hapo, Mtume (s.a.w.) alirudi kwa mkewe mwana Khadija (a.s.) akiwa amejawa
khofu kubwa. Alipoingia ndani alijitupa chini na huku akilalamika:
"Nifunikeni, nifunikeni!!" Alipotulia akasema: "Ninaogopa sijui
kitanipata nini?!" Khadija akamtuliza: "Sivyo! Wallahi Mwenyeezi
Mungu hatakuangamiza abadani, wewe unaunga udugu, unavumilia matatizo,
unasaidia wanyonge, unasaidia kuleta haki." Hapo Khadija akamchukua Mtume
akampeleka kwa Ibnu ammi yake Waraqa bin Nawfal (alikuwa mnasara, mwandishi wa
Injili kwa lugha ya kiibrania).
Walipofika
kwa Waraqa, Khadija akamwambia: "Ewe Ibnu ammi! Msikilize Muhammad aliyo
nayo." Waraqa akamuuliza, "una nini?" Muhammad (s.a.w.w)
akamwelezea yote kama aliyoyaona, Waraqa akamwambia: "Huyu ni Malaika
ambaye amepata kumteremkia vilevile Nabii Musa (a.s.) Ee!!!" Natamani kama
nitakuwa hai wakati watakapokufukuza watu wako!!! Muhammad (s.a.w) akashituka:
"Watanifukuza??" Waraqa akajibu: "Ndiyo, hakuna mtu yeyote
anayeleta jambo kama hili uliloleta wewe isipokuwa atapigwa vita na watu wake".
Taz:
Sahihi Bukhari J.I uk, 5-6
Sahihi
Muslim J. I uk, 97
Almuswannaf
J. 5 uk, 322
Tarikhut
Tabari J. 2 uk, 47
Enyi waislamu
wenzangu, mnaaminije hadithi hizi zenye kumshusha hadhi Mtume wetu kwamba yeye
alikuwa hajuwi kuwa yeye ni Mtume wa Allah mpaka aende kuambia na mkristo? Je hii
inaweza kuwa kweli? Story hii inamdhalilisha hata Jibril kwani tukikubali
hadith hizi itamaanisha kuwa Jibril ambaye anajulikana kuwa mwalimu wa mitume
wote alimbana na kumtesa mtume bila hata kumwambia yeye ni nani na wala
hakujitambulisha.
Sisi Mashia
tunaamini kuwa Jibril alipomtokea Mtume alijitambulisha kwake na pia Yeye
mwenyewe Mtume Mohammad (s.a.w.w) alijijua kuwa ni mtume na wala hakuhitaji
kwenda kuamiwa na wakristo kuwa wewe ni Mtume ndio woga aliokuwa nao ukaisha. Wewe
unasemaje?
Comments
Post a Comment