IKHITILAFU YA TAREHE YA KUZALIwA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

IKHITILAFU YA TAREHE YA KUZALIwA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
Katika kitabu cha historia cha Qadhi Husain Ibn Muhammad Diyar  Bakari al-Maliki inayoitwa Tareekh-e-Khamees, imeandikwa kwamba Mtume wetu alizaliwa mwezi kumi (10) Rabi-ul-Awwal,
na kwa mujibu wa walivyopokea wanahistoria wengine, tarehe ya kuzaliwa kwake ni kumi na mbili (12) Rabi-ul-Awwal
na wapo wanahistoria wengine ambao wamepokea kuwa  ilikuwa kumi na saba (17) Rabi-ul-Awwal.
Wote wanakubaliana kuwa ilikuwa mwaka wa tembo, yaani ‘aamul fiil.

Lakini wamekhitilafiana kuhusu huo mwaka unauwiana na mwaka gani wa kizungu yaani Gregorian. Wapo waliosema kuwa mwaka wa tembo unauwiana na mwaka 570 AD, wengine wakaandika kuwa mwaka huo ni sawa na mwaka 571 AD.

Comments