Assalaam Alaikum
Ndugu Waislaam, na wapenzi wa Ahlul-bayt wa Mtume (s.a.w.w), kwa leo si mbaya tukafaidika walau na Hadithi hii Tukufu ya ya aliye Rehema kwa walimwengu wote,Nabi wetu Muhammad (s.a.w.w), kama ifuatavyo:
Allama Zamakhshari na Razi, katika tafsiri zao za Qur'an Tukufu wameinakili hadithi hii tukufu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kama ifuatavyo:
((من مات على حب آل محمد مات شهيداً، الا و من مات على حب آل محمد مات مغفوراً له، الا و من مات على حب آل محمد مات تائباً، الا و من مات على حب آل محمد مات مؤمناً مستكمل الايمان...... الا و من مات على بغض آل محمد مات كافراً، الا و من مات على بغض آل محمد لم يشم رائحة الجنة.))
“Anayekufa akiwapenda Aali (kizazi) zake Muhammad hufa shahidi.
Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa akiwa amesha samehewa (madhambi yake).
Tambueni kuwa, anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad hufa (kifo cha) aliyetubia.
Tambueni kuwa anayekufa akiwapenda Aali zake Muhammad, hufa akiwa muumini, aliyekamilika imani (yake).
Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad, hufa akiwa kafiri.
Tambueni kuwa anayekufa akiwachukia Aali zake Muhammad hatoipata harufu ya pepo”.
---------------------------------------------------------------------------------
Tazama Hadithi hii katika sehemu hizi zifuatazo:
{Zamakhshari, Tafsirul Kash-shaf juzu ya 4, tafsiri ya sura Ash-shura, 42; 32, na
Fakhrud Din Arrazi, Tafsirul Kabir, Juzu ya 26, Ukurasa wa 165 – 166}.
Comments
Post a Comment