MAZUNGUMZO KATI YA MWALIMU WA KIIRAQ NA SHEIKH WA AL-AZHAR

MAZUNGUMZO KATI YA MWALIMU WA KIIRAQ NA SHEIKH WA AL-AZHAR

Mazungumzo yao yalihusu Misri na ulimwengu wa Kiarabu wa Kiislamu na kuhusu kushindwa kwa Waarabu na ushindi wa Wayahudi na mazungumzo yenye kuhuzunisha, Mwalimu wa kiiraq alisema kuwa sababu ya kushindwa kwa waarabu na waislamu mbele ya Israel ni kugawanyika kwa Waarabu na Waislamu kwenye dola ndogo ndogo na vikundi na Madh-hebu mengi licha ya wingi wao kwa idadi, basi hawana uzito wala mazingatio katika mtazamo wa maadui zao.

Walizungumza sana kuhusu Misri na Wamisri na walikuwa wakiafikiana juu ya sababu za kushindwa. Ndipo mwalimu aliongezea kwamba yeye anapinga mgawanyiko huu ambao wakoloni wanautilia mkazo miongoni mwetu ili iwe rahisi kwa kututawala na kutudhalilisha nasi bado tunatofautisha baina ya Mad-hab ya Malik na Mahanafi na alisimulia kisa cha kuhuzunisha kilichompata wakati alipoingia katika Msikiti wa Mahanafi mjini Cairo na akasali nao sala ya Alasiri kwa jamaa mara ghafla baada ya swala, mtu aliyekuwa kasimama pembeni yake akamwambia kwa hasira "Kwa nini hufungi mikono katika Sala'? yeye alimjibu kwa heshima na adabu kwamba, "Wafuasi wa Malik hawafungi mikono nami ni Malik" akamwambia "Nenda kwenye Msikiti wa Malik na ukaswali huko", basi alitoka hali ya kuwa amechukia tena mwenye uchungu kutokana na tendo hili lililomwongezea tatizo juu ya tatizo,

Basi mara yule Mwalimu wa Kiiraq akatabasamu na kumwambia kuwa yeye ni Shia. Kutokana na habari hii sheikh alichanganyikiwa na akasema bila kujali kwamba, "Lau ninge jua kuwa wewe ni Shia basi nisingezungumza nawe". Akasema, "Kwa nini?"
Sheikh akasema, "Ninyi siyo Waislamu kwani nyinyi mnamuabudu Ali ibn Abi Talib, na walio afadhali miongoni mwenu wanamuabudu Mwenyezi Mungu lakini nao hawaamini utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.) na wanao mshutumu Jibril na wanasema kuwa, yeye alifanya khiyana badala ya kupeleka utume kwa Ali akaupeleka kwa Muhammad." Na aliendelea kuzungumza mambo kama haya wakati ambapo mwalimu alikuwa akitabasamu na wakati mwingine alikuwa akisema, "lahaula Walaquwata Illa Billah" Ishara ya kuonyesha kushangazwa.

Sheikh alipomaliza maneno yake, aliuliza tena, "Wewe ni mwalimu unayesomesha wanafunzi?" sheikh akasema, "Ndiyo" akasema "Basi ikiwa fikra za Walimu ziko katika hali hii hapana lawama kwa watu wengine wa kawaida ambao hawana elimu".

Sheikh akauliza, "Unakusudia nini?" Alijibu, "Samahani, lakini ni wapi ulikoyapata madai haya ya uongo?"
Sheikh akajibu, "Katika vitabu vya historia ambavyo ni mashuhuri kwa watu wote".

Mwalimu akasema, "Tuachane na watu wote lakini ni kitabu gani cha historia ulichokisoma?"

Hapo sheikh alianza kuorodhesha baadhi ya vitabu kama vile FaJ-rul-Islam na Dhuhal-Islam na Dhuhri Al-Islam vya Ahmad Amin na vyenginevyo.

Mwalimu akasema, "Tangu lini Ahmad Amin amekuwa ndiyo hoja dhidi ya Mashia? akaongeza kusema hakika uadilifu na ukinzani ulio sawa ni kuyabainisha mambo kutoka katika rejea zao asilia zilizo mashuhuri".

Sheikh akasema, "Basi nitawajibika vipi kubainisha jambo ambalo linaeleweka kwa watu wote?"

Mwalimu akasema, "Huyu Ahmad Amin yeye mwenyewe alizuru Iraq nami nilikuwa miongoni mwa walimu waliokutana naye huko Najaf, na tulipomlaumu kuhusu maandiko yake juu ya Shia, aliomba radhi kwa kusema kuwa, mimi sina chochote ninachokijua juu yenu, na kwa hakika sijawahi kukutana na Shia hapo kabla na hii ndiyo mara yangu ya kwanza kukutana na Shia."

Sisi tulimwambia, "Huenda udhuru ulio utoa ni jambo baya zaidi kuliko kosa ulilolitenda kwani ni vipi ulikuwa hujui chochote kutuhusu siye nawe ukaandika kila kitu kibaya dhidi yetu?"
Kisha aliendelea akasema, "Ewe ndugu yangu sisi tutakapoyahukumu makosa ya Wayahudi na Wakristo kwa kutumia Qur'an tukufu ambayo kwetu sisi ni hoja madhubuti, basi mtazamo wetu huu utakuwa dhaifu kwa sababu wao hawaikubali Qur'an, na hoja yetu itakuwa madhubuti yenye nguvu tu ikiwa tutayabainisha makosa yao kwa mujibu wa vitabu vyao wanavyoviamini na hili litakuwa katika mizani ya "Ameshuhudia shahidi kutoka kwao wenyewe". (12:26)

Maneno yake yalitua ndani ya moyo wa sheikh kama yanavyoshuka maji katika moyo wa mtu mwenye kiu na alijikuta akibadilika kutoka katika hali ya mpinzani na kuelekea kwenye hali ya mtu mwenye kutafuta na kuchunguza, kwani (maneno yake) yalikuwa na mantiki iliyosalimika na ni hoja yenye nguvu, basi hakuwa na budi isipokuwa kutulia kidogo na kumsikiliza,
na ndipo sheikh alipomuuliza mwalimu, "Kwa hiyo nawe ni miongoni mwa wanao itakidi ujumbe wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.)?"

Akanijibu, "Na Mashia wote ni kama mimi wanaitakidi hivyo na ni juu yako wewe ndugu yangu kulithibitisha hilo wewe mwenyewe ili usiwe na shaka na jambo hili na usiwadhanie nduguzo Mashia dhana mbali mbali kwani baadhi ya dhana ni makosa" Na aliendelea kusema, "Na ikiwa kweli unataka kujua ukweli na kuyaona hayo kwa macho yako na moyo wako Uyakinishe basi mimi nakualika utembelee Iraq na ukutane na Wanachuoni wa Kishia na watu wa kawaida na ndipo Utakapo ufahamu uongo wa watu wenye dhamira mbaya".

Hivyo nami nasema kuwa kabla hujaanza kumtuhumu mtu mtembelee na muulize mwenyewe na visome vitabu vyake. Kwa misingi hii ninawaalika mawahhabi na masalafi katika vituo vyetu vya kishia ili wajifunze Ushia kwanza halafu ndipo wapate hoja za kupambana na ushia badala ya kuongea uzushi.

Comments