KATIKA ARDHI YA MINA
Mahujaji walikuwa wamekusanyika
Mina. Imam Sadiq (a.s.) na maswahaba wake walikuwa wameketi sehemu fulani
wakila zabibu zilizokuwa zimeandaliwa mbele yao.
Muombaji alitokea na kuomba
sadaka. Imam alichukua zabibu na kumpa lakini alikataa kuchukua na akaomba
pesa, Imam alimwambia kuwa amsamehe kwa kuwa hakuwa na pesa za kumpa. Muombaji
yule akaenda zake akiwa amekasirika.
Baada ya kwenda hatua chache
alijiwa na wazo na akarudi na kuomba zile zabibu. Imam sasa akakataa kumpa zile
zabibu pia.
Muda mfupi baadaye muombaji mwingine
alitokea na Imam alichukua zabibu ili ampatie. Alizichukua huku akisema,
“Namshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote na ambaye amenipa riziki
yangu.”
Kwa kusikia matamshi hayo Imam
alimwambia asubiri na akamuongezea zabibu zingine. Maskini yule alimshukuru
Mwenyezi Mungu kwa mara ya pili.
Imam alimwabia tena asubiri
huku akigeuka kwa mmoja wa marafiki zake na kumuuliza, “Una kiwango gani cha
pesa?” Bwana yule alitafuta mfukoni mwake na akapata takriban dirham ishirini
ambazo alimpa yule muombaji kwa amri ya Imam.
Masikini yule alimshukuru
Mwenyezi Mungu kwa mara ya tatu huku akisema “Shukrani zote zimuendee Mwenyezi
Mungu, Ewe Mungu wewe ndio mpaji na hauna mshirika.” Kusikia maneno hayo Imam
alivua joho lake na akampa muombaji huyo. Hapo mwombaji alibadilisha shukrani
zake na kuzungumza mambo ya ziada ya kumshukuru Imam mwenyewe. Kisha Imam
hakumpa kitu kingine na muombaji akaondoka zake.
Marafiki na maswahaba zake
ambao walikuwa mahali pale walisema: “Tulidhani kuwa kama masikini huyo
angeendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kama hapo awali, Imam angeendelea kumpa
vitu zaidi na zaidi. Lakini alipobadilisha matamshi yake na kumshukuru Imam
mwenyewe Imam hakuendelea na usaidizi wake.
Comments
Post a Comment