UTARATIBU WA KUWASULUHISHA WATU

UTARATIBU WA KUWASULUHISHA WATU

Wakati fulani, enzi za Imam Sadiq (a.s), Abu Hanifa, mtawala wa Hajjaaj, alikuwa na ugomvi na mkwe juu ya urithi. Mufadhal Ibn U’mar Kufi, mmoja wa masahaba wa karibu wa Imam Sadiq (a.s) alipita kwenye ugomvi huo. Aliposikia mabishano hayo alisimama na kusema kuwaambia hao wanaume wawili: “Twendeni nyumbani kwangu.” Walifanya kama alivyoomba.


Walipofika nyumbani aliingia ndani na muda mfupi baadaye alitoka na mfuko wenye dirhamu mia nne alizowapatia (hao) watu wawili na akawasuluhisha. Kisha akaeleza: “Hizi sio fedha zangu bali ni za Imam Jaafar Sadiq (a.s). Alinielekeza: “Wakati wowote utakapoona shia wetu wawili wakizozana juu ya fedha, wapatie fedha hizi na wasuluhishe.”

Comments