SALA YA ASUBUHI
1. Baada
ya kusema Iqamah, utanuwia sala kama hivi:-
Nasali Sala ya Asubuhi Rakaa mbili kurbatan ilallahi Taala
Nasali Sala ya Asubuhi Rakaa mbili kurbatan ilallahi Taala
2. Utasema' Allahu Akbar'
3. Utasoma sura ya Al-hamdu:
BISMILLAHIR
RAHMAANIR-RAHIM. ALHAMDU LILLAHI RABBIL – ALAMIIN. ARRAHMANIR RAHIIM. MAALIKI YAWMIDDIIN.
IYYAKA NAABUDU WAIYYAKA NASTAIIN. IHDINAS SIRAATWAL MUSTAQIIM, SIRAATWA
LLADHIINA AN’A AMTA ALAYHIM, GHAYRIL MAGH-DHUBI ALAYHIM WALADH - DHWAALLIIN.
Tafsiri
yake ni kama hivi:
Kwa jina la Allah Mwenye
rehema za dunia na rehema za Akhera.
Kila sifa nzuri inamstahili
Alla {Mungu} mlezi wa viumbe vyote.
Mwenye rehema za dunia na
akhera.
Mfalme wa siku ya Kiyama.
Wewe tu ndie tunae kuabudu,
na wewe tu ndio tunae kuomba msaada.
Tuongoze katika njia iliyo
nyooka sawa. Njia ya ambao ulio waneemesha, isiokuwa ya wale ulio waghadhibikia
juu yao wala wale walio potea.
4. Baadae utasoma, sura
nyingine yoyote kamili.
ni bora usome sura ya Tawheed:
ni bora usome sura ya Tawheed:
BISMILLAHIR
RAHMANIR RAHIIM
QUL HUWA
LLAHU AHAD. ALLAHUS SWAMAD. LAM YALID WALAM YUULAD. WALAM YAKULLAHUU KUFUWAN
AHAD.
Tafsiri
yake ni kama ifuatavyo:-
Kwa jina la Allah Mwenye
Rehma za dunia na Rehma za Akhera
Sema, yeye Mungu ni mmoja.
Mungu, Asiye hitaji, ambaye wote wanahitaji kwake.
Hakuzaa wala hakuzaliwa.
Wala hakuwa anaye fanana naye hata mmoja.
5. Kisha utasema' Allahu
Akbar' na utainama mpaka vifike viganja vyako magotini, utaweka juu yake na
utasema:-
SUBHANA RABBIYAL – ADHWIMI WA BIHAMDIHI
ALLAHUMMA SWALLI ALA MUHAMMADIN WA AALI MUHAMMAD
SUBHANA RABBIYAL – ADHWIMI WA BIHAMDIHI
ALLAHUMMA SWALLI ALA MUHAMMADIN WA AALI MUHAMMAD
{Ninamtukuza Mola wangu
Aliye mkubwa na ninataja sifa zake njema}
{Ewe Mwenyezi Mungu, Mrehemu
Muhammad na Ahli zake.}
6. Kisha utanyanyua kichwa
chako na utasimama, na kusema:-
Samiallaahu liman Hamida. Allahu Akbar.
Samiallaahu liman Hamida. Allahu Akbar.
{Mwenyezi
Mungu Anamsikia kila anayemshukuru}.
7. Kisha utasujudu;
utawekapaji lako la uso juu ya kidongo twahara au mfano wake, na hivyo hivyo
utaweka vitanga vyako na magoti na vidole gumba vya miguu ardhini, na
kusema:-'SUBHANA RABBIYAL A'LA WABIHAMDIHI ALLAHUMMA SWALLI ALAA MUHAMMADIN WA
AALI MUHAMMAD'
{Nataja
Utukufu wa Mwenyezi Mungu, Bwana wangu alie juu ' kabisa, na ninamshukuru}.
8. Kisha utanyanyua kichwa
chako na kukaa, na kusema: -
ALLAHU AKBAR, ASTAGH FIRU LLAHA RABBI WA ATUBU ILAYHI, ALLAHU AKBAR'
ALLAHU AKBAR, ASTAGH FIRU LLAHA RABBI WA ATUBU ILAYHI, ALLAHU AKBAR'
{Naomba
msamaha kwa Mwenyezi Mungu, Bwana wangu, na ninatubu kwake}.'
9. Kisha utasujudu sijda ya
pili kama ya mwanzo, utakaa baada yake,
kisha utasimama kwa Rakaa ya pili, utasema utaposimama.
BIHAULILLAHI WA QUWWATIHI AQUMU WA AQ-UD
{Kwa msaada na nguvu ya Mwenyezi Mungu nainuka na nakaa.}
kisha utasimama kwa Rakaa ya pili, utasema utaposimama.
BIHAULILLAHI WA QUWWATIHI AQUMU WA AQ-UD
{Kwa msaada na nguvu ya Mwenyezi Mungu nainuka na nakaa.}
10. Baada ya kusimama kutoka
Rakaa ya kwanza, utasoma sura ya Al-Hamdu na sura nyingine katika Rakaa ya pili
kama ulivyosoma katika Rakaa ya kwanza.
11. Baada ya kusoma Al-Hamdu
na sura, utaomba Dua na kunyanyua mikono mkabala wa uso, na utasema:-
'RABBANAA AATINA FIIDDUN’YAA
HASANATAN WA FIL AAKHERATI HASANATAN WAQINA
ADHABAN-NAR.'
{Ewe Mola
wetu; Tupe hapa duniani kila yaliyo mema, na utupe Akhera kila yaliyo mema, na
utukinge na adhabu ya moto.}
12. Kisha utarukuu,
kama ulivyofanya katika Rakaa ya kwanza, na utasujudu sijda mbili kama mwanzo.
13. Baada ya kukaa kutoka
sijda ya pili, utasoma Tashaahud kama ifuatavyo:-
ASH -
HADU AL LAA ILAAHA ILLALLAHU WAHDAHU LA SHARIKA LAHUU WA ASH - HADU ANNA
MUHAMMADAN ABDUHU WA RASULUH. ALLAHUMMA SWALLI ALAA MUHAMMADIN WA AALI
MUHAMMAD.
Tafsiri
yake ni hii:
Nakiri kuwa hapana Mola ila
Mwenyezi Mungu, yeye tu wala hana mshirika yeyote.
Na nakiri kuwa Muhammad
{s.a.w.w.} ni mtumwa na mjumbe wake.
Ewe Mwenyezi Mungu mpelekee
rehma Mtume wako Muhammad na Ahali zake.
14. Kishautasoma Salaam:-
ASSALAAMU
ALAYKA AYYUHANNABIYYU WARAHMA TULLAHI WA BARAKATU. ASSALAAMU ALAYNA WA ALA
IBADILLAHIS SALIHIIN
ASSALAAMU
ALAYKUM WARAHAMA TULLAHI WA BARAKATUH.
Tafsiri
yake ni kama ifuatavyo:-
Amani juu
yako Ewe Mtume Mtukufu, na Rehma ya Mwenyezi Mungu na baraka zake; Amani juu
yetu na juu ya viumbe wa Mungu watenda mema:
Amani juu
yenu na Rehma ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake.
15. Kisha utasema ALLAHU AKBAR, ALLAHU AKBAR, ALLAHU AKBAR.
16. Baada ya sala ni bora mno kusoma Tasbihi kama hivi: -ALLAHU
AKBAR {x34} AL-HAMDU LILLAH {x33} SUB HANA LLAH {x33}
Comments
Post a Comment