HAJJAAJ NA MUUZA MAZIWA

HAJJAAJ NA MUUZA MAZIWA
Siku moja Hajjaaj Ibn Yusuf Thaqafi, dikteta katili na waziri wa khalifa wa ukoo wa Abbas, Abd al-Malik ibn Marwaan alikuwa akitembea sokoni aliposhuhudia muuza maziwa akiongea peke yake.
Akiwa amesimama kwenye kona, Hajjaaj alimsikia akisema: “Nikiuza, maziwa haya, nitapata kipato kizuri. Nitaweka akiba kutokana na mauzo haya na mauzo yajayo mpaka nitakapokuwa na fedha za kutosha kununulia mbuzi. Kisha nitanunua kondoo jike na kutumia maziwa yake kuongeza mtaji wangu na ndani ya miaka michache, nitakuwa mtu tajiri ninayemiliki mbuzi wengi, ngo’mbe na aseti (nyinginezo).
Kisha nitamposa binti wa Hajjaaj, ambapo baada ya hapo nitakuwa mtu muhimu. Na ikiwa wakati wowote binti wa Hajjaaj ataonyesha uasi (kutotii) nitampiga teke kubwa kiasi cha kuvunja mbavu zake.” Aliposema hivi alipiga teke kwa mguu wake ambao kwa bahati mbaya uligonga dumu la maziwa, na hivyo kumwaga vyote vilivyokuwemo.
Hajjaaj alitokeza na akaamuru askari wake wawili kumlazimisha muuza maziwa alale chini na kumcharaza fimbo mia moja.
Muuza maziwa alilalamika, “Lakini ni kwa kosa gani unaniadhibu?”
Hajjaaj alijibu, “Je hukusema kwamba kama ungemuoa binti yangu ungempiga teke kubwa kiasi cha kumvunja mbavu zake? Sasa, kama adhabu ya teke hilo, lazima uonje fimbo mia moja.”
Rejea:
Daastaan – ha-e-Ustaadh, Jz. 1. uk. 48 4.

Comments