JINA LAKE NA NASABU YAKE.
Jina lake ni Mohammad bin Abdallah bin Abdul Mutwalib bin Hashim
bin Abdul Manaf bin Quswai bin Kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia kwa
mtume Ibrahiim (A.S)
MAMA YAKE.
Mama yake ni Amina binti Wahabi bin Abdul manafi bin Zuhra bin Kilaab.
KUNIA YAKE NI:
Abul qaasim, pia Abuu Ibrahiim.
JINA LAKE MASHUHURI.
1- Mustafa, na anayo majina mengine mengi yaliyo pokelewa
ndani ya Qur’ ani tukufu kama:
2- Khaatamun Nabiyyiin. 3- Al Ummiyyi. 4- Al Muzammil. 5- Al
Mudathir. 6- Al Mubiin. 7-Al Kariim.
8- An Nuur. 9- An Niima. 10- Ar Rahmaan. 11- Ash Shaahid.
12- Al Mubashir.13- An Nadhiir. 14- Abdur Rauuf. 15- Ar
Rahiim. 16- Ad Daai na mengine mengi.
TAREHE YA KUZALIWA KWAKE.
Alizaliwa tarehe 17 mwezi wa Rabiiul
awwal, mwaka wa tembo sawa na mwaka 571 H.D. kutokana na kauli
iliyo mashuhuri kwa mashia, na kauli nyingine inasema ya kuwa alizaliwa tarehe
12 mwezi wa Rabiul awwal mwaka huo huo.
SEHEMU ALIPO ZALIWA.
Alizaliwa katika mji wa Makkatul Mukarramah
ulioko katika nchi ya Saudi Arabia ya sasa.
KUPEWA KWAKE UTUME.
Ali pewa rasmi utume tarehe 27 mwezi wa
rajab katika mji wa Makka baada ya kutimiza miaka 40 ya umri wake
mtukufu.
MAFUNDISHO YAKE.
Mtume (s.a.w) alikuja na wito wa usawa kwa viumbe
wote, na alikuwa akilingania udugu, na msamaha kwa kila mwenye kuingia kwenye
Dini ya ki islaam, kisha aliweka sheria iliyo nyepesi, na kanuni za uadilifu
alizo zipokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu alie takasika, kisha waislaam wakazipokea
kutoka kwa Mtume (s.a w).
MIUJIZA YAKE.
Muujiza wake pekee wa milele na milele ni Qur’
ani tukufu; ama miujiza yake iliyo dhihiri mwanzoni mwa uislaam ni mingi sana kwani
haihesabiki.
Comments
Post a Comment