HISTORIA YA MTUME (S.A.W.W) MAPACHA WA ABDI-MANAF

Bwana Ibn Athir al-Jazari katika kitabu chake Tarikh al-Kamil anaandika kwamba Abdi-Manaf (Babu wa tatu wa Mtume wetu (s.a.w.w.)) alikuwa na watoto wawili Abdush-Shams na Hashim ambao walizaliwa mapacha kwa hali kidole cha mmoja wao kiligandana na kipaji cha mwenziwe. Walipofanyiwa kupasuliwa mahali pale paliposhikamana ikatoka damu nyingi. Wakasema watu: ‘hii ilionyesha kwamba baina ya ukoo wao patamwagika damu nyingi’.

Aliposhika Bwana Hashim mahala pa baba yake Abdi-Manaf kuwa yeye mkubwa wa kabila, basi Ummayah mtoto wa Abdush-Shams akaona wivu juu yake, hivyo uadui baina ya watoto wa Hashim na Ummayah ukaanzia hapa.

Katika kitabu cha tafsir mashuhuri kiitwacho Durr al-Mansur cha Jalaluddin Suyuti imeandikwa hivi kwamba Ibn Jaree, Ibn Mundhir, Ibn Abi Hatim, Tabrani, Ibn Mardwaih na Hakim wamehadithia kwa njia sahihi mbali mbali kwamba Ali ameeleza tafsiri ya aya hii: ‘Alam-Tara Ilal-Ladhiyna Bad-Daluu Nia-Matal-Laahi Kufra”. (Je, hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyeezi Mungu kwa
kufru) (Sura Ibrahim, Aya 28) hivi, “Wale waliobadili dini ya Mwenyezi Mungu kwa kukufuru ni wana (watoto) wa Umayyah na watoto wa Mugheera, ambao ni wenye kubobea kwa dhambi kuliko Quresh wote.”

Sijui itakuwaje kwa wafuasi wao? Kumbuka Uthuman bin Afan, Muawiyah bin Sufian, Yazid bin Muawiya n.k walikuwa bani Umayya yaani watoto wanaotokana na fitina hii iliyotajwa katika Qur’an tukufu. Bila shaka Mawahhabi na wapende kuua wote wanatokana na kizazi hiki au ni wafuasi wao. Mungu atuepushe kutokana na kukifuata kizazi hiki kilicholaaniwa.
Ameen. 

Comments