Imam Ali alijaaliwa kuwa mkono wa kuume wa Uislamu, na ngao na
kingio la Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) Takdira au maajaliwa yake yalikuwa
kiungo kisichotenganishwa na takdira ya Uislamu, na maisha ya Mtume wake.
Alikuwepo katika kila hali ya mambo katika historia ya harakati hii, na
alishika nafasi ya kuwa nyota ndani yake. Ilikuwa, kwa dharura, ni nafasi
ambayo yeye pekee ndiye angeweza kuishika. Aliakisi "taswira" ya
Muhammad (s.a.w.w). Kitabu cha Allah (s.w.t.) chenyewe kimemuita
"nafsi" au mwandani (nafsi ya pili) ya Muhammad katika Aya ya 61 ya
Sura ya tatu, na alionyesha jina lake maarufu toka upande mmoja hadi mwengine,
wa historia.
Katika miaka ijayo, muundo wa ufanyaji kazi pamoja wa Muhammad na
Ali - amir na mfuasi - utakuja kuweka "Ufalme wa Mbinguni" katika
ramani ya dunia, HATA KAMA WANAFIKI WANALIPINGA HILO NA KUANZISHA TAWALA ZAO ZA
KUCHINJA WATU BILA HURUMA NA KUWADHALILISHA WANADAMU.
Comments
Post a Comment