ISRA NA MIRAJ: Bayt al Ma’mur

Mtume Mohammad (s.a.w.w) anaendelea kuhadithia, nilipofika mbingu ya saba niongozwa na Jibrail kuingia Bayt al-Ma’mur, kundi la marafiki wangu niliokuwa nimefuatana nao walikuwemo waliovaa nguo kuukuu na wengine nguo mpya, waliovaa nguo mpya tu ndio walioruhusiwa kuingia katika eneo hilo.
Hapa nikaswali rakaa mbili kumshukuru Allah, kisha nikasonga mbele na kuona mito miwili, mto al-Kawthat na mto wa Rahma. Nikanywa maji katika mto al-Kawthar na kuoga katika mto wa Rahma. Kisha niliongozwa mpaka peponi. Katika eneo Fulani la pepo niliiona nyumba yangu na ya mke wangu (Khadija).
Katika eneo jingine la pepo nimuona mtumishi (mwanamke mzuri) wa Allah akiwa anaoga, nikamuuliza ewe mtumishi wa Allah, ni nani wewe? Akajibu mimi niko hapa kwa ajili ya Zaid bin Harith (nipofika Maka nilimtaarifu Zaid kuhusu Baraka hizi alizopewa na Allah)
Kisha niliuona mti mkubwa ambao kama ndege akiuzunguka kwa kasi kwa miaka 700 asingeweza kukamilisha mzunguko wake. Na mti huu matawi yake yameenea na kuifikia kila nyumba ya peponi. Nikamuuliza Jibrail kuhusu mti huu. Akanijibu kuwa huu ni mti wa Tuba ambao Allah amesema katika Qur’an
"...Tuba itakuwa ndio marejeo yao yaliyo bora kabisa. " kila nyumba ya peponi iko chini ya kivuli cha mti huu.  
Kisha Jibrail akasema kuwa Allah ameweka pazia kiasi kwamba hakuna kiumbe chenye uwezo wa kumwona.


Soma Bihar al-Anwar, Vol. 18, p. 327-328, Bab 3 - Ithbaat al-Mi`raaj wa ma`anaahu wa kayfiyyatuhu wa sifatuhu wa ma jaraa feehi wa wasf al-buraaq, Hadith 34.

Comments