Tarehe ya tukio hili
imeandikwa na wanahistoria maarufu wa kiislamu wawili Ibn Ishaq na Ibn Hisham
ya kwamba ilikuwa mwaka wa 10 baada ya tangazo la utume wa Muhammad (s.a.w.w).
lakin Baihaqi ameandika kuwa tukio hili lilitokea mwaka wa 12 baada ya tangazo
la utume. Na wengine.
Huenda tukio hili
lilitokea mara mbili, lakini tukio hili liliambatana na agizo la swala tano,
bila shaka tukio hili limetokea kabla ya kifo cha mzee Abutalib aliyefariki
mwaka wa kumi.
Hadith: JIWE LA JAHANAMU
Mtume (s.a.w.w)
anahadithia kuwa alipokuwa mbinguni alisikia sauti ya kutisha, akauliza ndipo
alipoambiwa kuwa hiyo ni sauti ya jiwe lilirushiwa ndani ya moto wa Jahanamu
miaka 70 iliyopita na sasa ndio kwanza linatua chini ya Jahannamu. Kutokana na
tukio hili Mtume hakuwahi kuonekana akicheka tena.
Kisha
anasema tuliendelea na safari yetu ambapo nilimuona malaika aitwaye Ismail. Yeye
ni mhudumu wa Khitfah ambayo Qur’an inasema kuwa baadhi ya wanaohitaji kuiba
siri za mbinguni hudhibitiwa kwa ndimi za moto. Ismail ni kiongozi wa malaika
wenziwe 70,000. Ismail alimuuliza Jibrail kuwa ni nani huyu? Akajibiwa huyu ni
Muhammad ambaye amepewa ujumbe na Allah.
Mlango ulifunguliwa
tukaingia mbinguni. Nilimsalimia na nikamuombea msamaha. Naye alinisalimia na
kumuomba Allah anihurumie. Kisha akasema karibu ewe Mtume mkuu, wakati huo
kundi la malaika lilinisalimia. Wote walikuwa wanatabasamu. Isipokuwa mmoja
ambaye alikuwa amekaa katika muundo wa kujificha, jina lake ni Khazin ambaye
alikuwa na huzuni tena akilia. Jibrail akasema kuwa huyu ndio muwashaji wa Moto
wa Jahanam, tokea Mwenyezi Mungu alipomteua kuwa muwashaji wa moto wa Jahanamu
hajacheka tena mpaka leo. Kila siku hasira zake dhidi ya waovu zinaongezeka na
kupitia malaika huyu waovu wataadhibiwa na Allah. Nilimsalimia naye
akanisalimia kisha akaniambia kuwa mimi ni mtu wa peponi, kisha aliniuliza kama
ninataka kuuona moto wa Jahanamu, Jibril akasema muoneshe.
Khazin
alifungua mlango wa Jahannam na moto ukasambaa mpaka angani kiasi kwamba
nilidhani kuwa ndimi hizi za moto karibia zitanifikia.
Jibril alimwagiza
Khazin afunike Jahanam, hivyo ikafunikwa.
Soma Bihar al-Anwar, Vol. 18,
p. 320-321, Bab 3 - Ithbaat al-Mi`raaj wa ma`anaahu wa kayfiyyatuhu wa sifatuhu
wa ma jaraa feehi wa wasf al-buraaq, Hadith 34.
Comments
Post a Comment