Mtume (s.a.w.w)
anaendelea kutuhadithia: tulifika eneo linaloitwa Sidratul Muntaha. Eneo hili
lina mti ambao jani lake moja ni kubwa kiasi cha kufunika taifa zima. Kisha tukaenda
katika eneo ambalo Allah amesema katika Qur’an kuwa … kiasi kwamba alikuwa
umbali wa mita mbili au chini yake kwa ukaribu. Kisha Allah aliita, Mtume ameamini mambo ambayo Mola wake
amemfunulia.
Kwa niaba ya umma wangu
niliitika, na waumini wote wanamwamini Allah, malaika wake, vitabu vyake na
mitume wake, hatutofautishi kati ya Mitume. … umma wangu wanasema, … tumesikia
na tunatekeleza, Mola wetu. Hivyo tunakuomba msamaha nasi tunakutegemea wewe.
Allah (S.W)
akasema siwezi kukulazimisheni kufanya jambo isipokuwa linalingana na uwezo
wako. Kisha nikasema, Mola wetu, usituadhibu tutakapo sahau au kukosea. Allah (S.W)
akajibu, sitokuadhibuni.
Kisha nikaendelea,
ewe Mola wetu, usitutwishe mzigo mkubwa kuliko ulivyowatwisha waliotutangulia.
Allah akajibu, sitokutwisheni mzigo.
Nikasema
kwa mara nyingine, Mola wetu usitulazimishe kufanya yale ambayo hatuna uwezo wa
kuyafanya, tusamehe, tunaomba ulinzi wako na huruma yako. Hakika wewe ndio
mlezi wetu, hivyo tusaidie tuweze kuwashinda makafiri.
Mwenyezi
Mungu mtukufu akasema hakika hayo ndio niliyokupa wewe na umma wako.
Soma; Bihar
al-Anwar, Vol. 18, p. 328-329, Bab 3 - Ithbaat al-Mi`raaj wa ma`anaahu wa
kayfiyyatuhu wa sifatuhu wa ma jaraa feehi wa wasf al-buraaq, Hadith 34.
Comments
Post a Comment