Mtume baada ya kwa miaka kumi ya kuishi mjini
Madina ambapo Mtume (s.a.w.) aliugua kwa mara ya mwisho. Huu ulikuwa ni muda
mbaya sana kwa familia yake. Hadhrat Ali (a.s.) alikaa karibu na Mtume (s.a.w.)
kwa wakati wote wa ugonjwa wake na Mtume (s.a.w.) hakupendelea Hadhrat Ali
(a.s.) aachane naye hata kwa muda mfupi tu. Hatimaye, Mtume (s.a.w.) aliaga
dunia na kurudi kwa Bwana Wake. Kabla hajafa Mtume (s.a.w.) alimtaka Hadhrat
Ali (a.s.) asogee karibu naye, akamkumbatia na akazungumza naye kwa muda mrefu
akiwa na madhumuni ya kumpa maagizo ya mwisho. Hata baada ya Mtume (s.a.w.)
kumaliza mazungumzo yake na Hadhrat Ali (a.s.) hakumwachilia aende, bali
aliendelea kumshika mkono na kuuweka kifuani pake na roho ya Mtume (s.a.w.)
ilipotoka mkono wa Hadhrat Ali (a.s.) ulikuwa bado upo kifuani pake.
Comments
Post a Comment