(1) al-Fadhl bin
Shaadhaan: Huyu ni kati ya wanazuoni wakubwa wa Kishia aliyeishi
katika karne ya tatu ya Hijria. Katika kitabu chake kiitwacho al-lidhaah, katika
kukataa baadhi ya maoni ya wanazuoni wa Kiwahhabi wa zama zake kwamba Qur'ani
Tukufu imepotolewa, amesema:
Lakini wale ambao, kwa kutaja Hadith kama hizo, wadhania kwamba
nassi ya Qur'ani imepotolewa, bila shaka wanakosea.
(2) Abu Ja'far Muhammad b. Ali b. Baabawayh al-Qummi: Mwanachuoni
huyu ni maarufu zaidi kwa jina la al-Shaykh as-Saduq na
alifariki dunia katika mwaka 381 Hijriyyah. Yeye amesema hivi katika kitabu
chake kiitwacho al-l'tiqaadaat:
lmani yetu ni kwamba Qur'ani ambayo Mwenyezi Mungu s.w.t.
amemteremshia Mtume Wake Muhammad s.a.w.w, ni hii hii iliyo baina ya majalada
mawili na iliyomo mikononi mwa watu; si zaidi ya hiyo... Na yeyote
anayetusingizia kwamba twasema zaidi ya hivyo, basi huyo ni mwongo.
(3) Sayyid al-Murtadhaa Ali bin al-Husayn al-Muusawi
al-Alawi: Huyu ni mwanachuoni mwingine mkubwa wa Kishia aliyefariki
dunia katika mwaka 436 Hijiriyyah. Yeye, katika kujibu maswali ya Taraabulusiyyaat, amesema:
Ujuzi wa kwamba mapokezi ya Qur'ani ni sahihi ni kama ujuzi wa
nchi na miji, matukio makubwa makubwa ya kihistoria, vitabu mashuhuri, na
mashairi yaliyoandikwa na Waarabu. Hili ni kwa sababu hamu na sababu za
kuinakili na kuihifadhi Qur'an zilishitadi na kufikia kiwango ambacho
hakikufikiwa na hayo mengine tuliyoyataja.... katika zama za Mtume wa Mwenyezi
Mungu s.a.w.w. Qu'rani ilikuwa ni mkusanyo uliotungamanishwa kama ulivyo
hivi sasa. Mtume s.a.w.w. alikuwa hata ameteua masahaba wa kuihifadhi
kwa moyo na kuilinda. Pia ilikuwa ni desturi (ya baadhi ya masahaba) kuisoma
mbele zake ili kuhakikisha kuwa ndivyo. Kikundi cha masahaba, kama vile
Abdullah b. Mas'ud, Ubayy b. Ka'b, na wengineo walikiihitimisha Qur'ani mbele
za Mtume s.a.w.w. hitima kadha wa kadha. Na yote haya yaonyesha, hata kwa
taamuli ndogo, kwamba Qur'ani ilikuwa ni mkusanyo uliopangwa; haukukatika
kipande wala haukutawanyika.... Na kwamba yeyote katika Imamiyya (Shia
Ithnaashari) au Hashwiyya (wasiokuwa Shia), anaye amini
kinyume cha hivyo, basi kinyume hicho chatokana na watu wa Hadith walionakili
Hadith dhaifu wakidhania ni sahihi; hali Hadith dhaifu kama hizo haziwezi
kulirudi jambo ambalo usahihi wake unajulikana kwa njia isiyo na shaka.
Maneno hayo unaweza kuyaona katika Majma'ul Bayaan, Juzuu
ya Kwanza, uk. 15.
Comments
Post a Comment