OMAR BIN KHATAB AIPINGA QUR’AN
Katika zama za ukhalifa wa Umar bin Khatab, sahaba mmoja alimuuliza, “Ewe Amirul-muumin, mimi nimepatwa na janaba lakini sikupata maji.” Umar akamwambia, “Usisali”. Hapo Ammar bin Yasir alilazimika kumkumbusha kutayamam, lakini Umar hakuafikiana naye kwa hilo na akamwambia Ammar, “Tutakubebesha jukumu kwa yale uliyojibebesha.”
Katika zama za ukhalifa wa Umar bin Khatab, sahaba mmoja alimuuliza, “Ewe Amirul-muumin, mimi nimepatwa na janaba lakini sikupata maji.” Umar akamwambia, “Usisali”. Hapo Ammar bin Yasir alilazimika kumkumbusha kutayamam, lakini Umar hakuafikiana naye kwa hilo na akamwambia Ammar, “Tutakubebesha jukumu kwa yale uliyojibebesha.”
Basi
yu wapi Umar na kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume? Je sio
Mtume aliyewafundisha Masahaba namna ya kutawadha na kutayamam? Cha kushangaza
kuna watu wanaompandisha cheo mtu huyu asiyekuwa na ujuzi wa Uislamu na kumwita
al-farooq na wakati Umar mwenyewe anakiri kuwa hakuwa na elimu kuliko wengine. Na
pia alisema mara nyingi, “Lau si Ali, basi Umar angeangamia, na mpaka anakufa
hakuwahi kutambua maana ya Al-kalalah ambayo alihukumu kwa hukumu nyingi
tofauti tofauti kama inavyoshuhudia Historia. Omar waliwapiga watu waliomuuliza
tafsiri ya Qur’an na masuala mengine ya kisheria.
Soma:
1. Tarikh Al-Yakubi juz. 2
uk. 106
2. Futuhul Buldan uk 437
3. Sahihi Bukhari juz. 1 uk.
52
Tumesimuliwa
masimulizi mengi juu ya Ushujaa wa Umar bin Khatab lakini ukifuatilia Historia
utagundua kuwa Umar alikuwa shujaa wa kuuwa waislamu wenzake na watu wasiokuwa
na hatia. Lakini anapokuwa vitani alikuwa ni mwoga kweli kweli.
Omar
na wenziwe walikimbia katika vita vya Uhud, na Hunain. Pia Mtume alipomtuma
katika vita vya Khaibar alirudi bila ushindi na hata katika vikosi vidogo
vidogo alivyoshiriki hakupewa uongozi. Kwa mara ya mwisho aliagizwa na Mtume
kuwa chini ya jeshi lililokuwa linaongozwa na kijana wa miaka 18 yaani Usamah
bin Zaid bin Harith.
Umar
alithubutu kumtisha Fatumah bint Rasulullah kuwa kama wasipotoka kwenda
kukubali utawala wa Abubakar basi ataiunguza nyumba yake. Kama haitoshi alidiriki
kuwa dhidi ya kitabu cha Allah na Sunnah za Mtume wake, akahukumu katika zama
za Ukhalifah wake, hukumu zinazokwenda kinyume na Qur’an na Sunnah tukufu.
Soma:
1. Tarikh At-Tabari na Tarikh
ibn Al-Athir
2. Al-Imamah was-Siyasah cha
ibn Qutaibah
3. An-Nas wal-Ijtihad
Uko
wapi ucha Mungu wa Umar enyi watu? Kama kiongozi yuko hivi itakuwaje kwa
wanaomfuata? Tafakari, chukua hatua.
Mambo
mengi mazuri kumhusu Umar yaliandikwa na watu aliowaajiri ili kuhalalisha
ufedhuli na dhuluma zake dhidi ya Mtume na Ahlulbayt wake na hata waislamu kwa
ujumla. Lakini mtu atakayesoma vitabu kwa makini, uovu wa Umar haufichi hata
ufanyeje.
Comments
Post a Comment