QUR'ANI TUKUFU IMEHIFADHIKA, HAIBADILIKI

Mwenyezi Mungu s.w.t. amesema:
(i) Hakika Sisi ndisi tuliouteremsha Ukumbusho (huu), na hakika Sisi ndio Wenye kuulinda. (Sura 15:9)
(ii)... Bila shaka hicho ni Kitabu Kitukufu. Hakitajiliwa na batili mbele yake wala nyuma yake; ni wahyi utokao kwa Mwenye hekima, Asifiwaye. (Sura 41:41-42)
Hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu yanayotuthibitishia kwamba Qur'ani ni kitabu kilichohifadhiwa na kila aina ya nyongeza, upungufu au mabadiliko. Waislamu wote - wa zama zote na nchi zote - wanaamini kwamba hii Qu'rani tuliyonayo leo ndiyo ile ile iliyokuwako zama za Mtume s.a.w.w., na ndiyo hii hii itakayokuwako mpaka Siku ya Kiyama, Kwa hivyo, mtu ye yote atakaye amini kinyume cha hivyo, huyo si Mwislamu.

Waislamu wote tutegemee marejeo ya elimu na sheria toka kwenye kitabu hiki kitakatifu. Isipokuwa tujue tafsiri sahihi za aya kwani kuna mtindo ambapo watu wanaichukia Qur’an na kuipa tafsiri potofu. Qur’an ikitumika kwa usahihi, tutapata nguvu na tutaiongoza dunia kwa idhini ya Allah (s.w).

Comments