TUKIO LA ISRA NA MIRAJ: USHAHIDI KATIKA QUR’AN

Tukio hili la Mtume kwenda mbinguni limethibitishwa na Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitukufu katika surah mbili yaani Isra (sura ya 17) na Najm.
Katika Isra Allah anasema, “sifa ni za Allah aliyemsafirisha mja wake kutoka Msikiti Mtakatifu Haram hadi Mskiti wa Aqsa, palipobarikiwa ili kumwonesha alama na dalili zetu. Kwa hakika Yeye ni msikivu na mwenye kuona”.
Kutokana na aya hii,tunapata ushahidi kuwa Mtume (s.a.w.w) alisafiri mzima mzima na wala sio ndoto kama baadhi ya watu wanavyodai. Lakini pia tunaona kuwa safari hii ni ya kimiujiza ya mtu kusafiri toka Maka hadi Yerusalem na kurudi kwa usiku mmoja tu. Japokuwa aya inaelezea safari ilianzia Maka na kuishia Yerusalem lakini ni ukweli kuwa alipofika Yerusalem alipaa angani ili Allah akamuonesha ukubwa wa uumbaji wake.
Katika Surat Najm utapata maelezo mapana zaidi kuhusu safari hii tukufu.


Mtume (s.a.w.w) alipofika aliwaambia Maquraish kuwa alimuona malaika Jibrail katika umbo lake halisi. Maqraish walisimama na kuanza kumpinga. Allah analithibitisha hili kwa aya zifuatazo, “mtampinga kwa kitu alichokiona? Kwa hakika alimuona (Jibrail) pembeni ya mti (mbingu ya saba) jirani na Pepo. Wakati ambapo mti ulikuwa umefunikwa, macho ya (Muhammad) hayakumdanganya. Kwa hakika aliona alama kuu kabisa za kuthibitisha uwepo wa Mwenyezi Mungu. (soma Surat Najm)

Comments