nimeleta ushahidi wa maneno ya Imam
Ali mwenyewe ya kuwa alikuwa akiamini kuwa Ukhalifa ni wake ingawa alikubaliana
na wenzake baada ya fujo na kutoelewana juu ya suala hilo kutokea: Je,
Wanachuoni wa Ki-Sunni wanaliona tukio hili kuwa ni sahihi?
Idadi ya mabingwa wa Ki-Sunni ambao wamesimulia tukio hili kwa urefu na kwa Mukhtasari, hushangaza akili! Tukio hili la kihistoria lilisimuliwa na Masahaba 110 wa Mtukufu Mtume (s.a.w) wafuasi wa Masahaba 84 na kisha likasimuliwa na mamia mengi ya wanachuoni wa ulimwengu wa Ki-Islamu, kuanzia karne ya kwanza mpaka kwenye karne ya kumi na nne AH (Karne ya 7-20 AD)
Takwimu hizi hujumuisha tu wapokezi waliomo katika simulizi zilizoandikwa na wanachuoni wa Ki-Sunni! Sehemu ndogo ya vyanzo hivi inatolewa hapa chini. Wengi wa wanachuoni hawa hawakunukuu tu tangazo hili la Mtume (s.a.w) bali vile vile wanaliita sahihi: " al-Hakim al-Naysaburi, al-Mustaddrak 'ala al-Sahihyn (Beirut), juzuu 3, uk. 109-110, uk. 133, uk. 148, uk. 533. Ameelezea kwa uwazi kwamba hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa vigezo vya Bukhari na Muslim. Al-Dhahabi alithibitisha hukumu yake.
" al-Tirmidhi, Sunan, (Cairo), juzuu 5, uk. 633.
" Ibn Majah, Sunan, (Cairo, 1952), juzuu 1, uk. 45.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Fath al-Bari bi Sharh Sahih al-Bukhari, (Beirut, 1988), juzuu 7, uk. 61.
" al-'Ayni, 'Umdat al-Qari Sharh Sahih al-Bukhari, juzuu 8, uk. 584.
" al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, juzuu 2, uk. 259 na uk. 298.
" Fakhr al-Din al-Razi, Tafsir al-Kabir, (Beirut, 1981), juzuu 11, uk. 53.
" Ibn Kathir, Tafsir Qur'an al-Adhim, (Beirut) juzuu 2, uk. 14
" al-Wahidi, Asbab al-Nuzu, uk.l64.
" Ibn al-Athir, Usd al-Ghaba fi Ma'rifat al-Sahaba, (Cairo, 1932), juzuu 3, uk.92.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Tahhdib, (Hyderabad, 1325), juzuu7, uk. 339.
" Ibn Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, (Cairo, 1932), juzuu7, uk. 340, juzuu 5, uk. 213.
" al-Tahawi, Mushkil al-Athar, (Hyderabad, 1915), juzuu 2 uk. 308-9.
" Nur al-Din al-Halabi al-Shafi'i, al-Sirah al-Halabiyya, juzuu3, uk. 337.
" al-Zrqani, Sharhe al-Mawahib al-Ladunniyya, juzuu 7, uk. 13
Angalieni basi msidanganywe na waliopumbazwa na tungo za kimadhehebu na Khawarij wa Akheri zamaan kama Mtume alivyotuagiza kwa kutubashiria kutokea kwa watu kama hawa wenye kuukana ukweli hata kama wanajuwa kuwa wanayoyasema si sahihi. Nakuomba usiwe katika kundi hilo inshaallah na urudi katika haki na usisimame na uongo inshaallah.
Aya ya 55-56 ya Sura ya 5 (Al-maidah) imeshuka kwa shani ya Imam Ali (a.s), jambo hili najuwa unaweza kulikataa lakini huwezi kulifuta katika Vitabu vilivyoandikwa kabla ya wewe hujazaliwa. Jambo hili limetajwa katika Vitabu vya Shia na Sunni, miongoni mwa Vitabu vya Shia vilivyotaja jambo hili ni: Bihar al-Anwar, cha Allama Majlisi, Tafseer al-Mizan, cha Allama Tabatabai, Tafseer al-Kashaf, cha Allama Muhammad Jawad Mughniyah, al-Ghadir, cha Allama Abdul Husain Ahmad al-Amini na Ithbat al-Hudate, cha Allama Muhammad Ibn Hasan Amuli.
Amma Vitabu vya Sunni vilivyosema kuwa tukio la aya hiyo lilikuja kwa shani ya Imam Ali (a.s) ni vingi sana, miongoni mwa Vitabu hivyo ni:
(1) Tafsir al-Kabir, ya Imam Ahmad Ibn Muhammad al-Tha'labi, chini ya maelezo ya aya ya Sura ya 5 aya ya 55-56.
(2) Tafsir al-Kabir, ya Imam Ibn Jarir al-Tabari, jalada la 6, kurasa za 186, 288-289
(3) Tafsir Jamiu al ahkam al-Quran, ya Imam Muhammad Ibn Ahmad Qurtubi, jalada la 6, uk. wa 219
(4) Tafsir al-Khazin, jalada la 2, uk. wa 68
(5) Tafsir al-Durr al-Manthoor, ya Imam al-Suyuti, jalada la 2, uk. wa 293-294
(6) Tafsir al-Kashshaf, ya Imam al-Zamakhshari, Chapa ya Misri mwaka 1373, jalada la 1 uk. wa 505 na 649
(7) Asbab al-Nuzool, cha Imam Jalaluddin al-Suyuti, Chapa ya Misri ya mwaka 1382, jalada la 1 uk. wa 73, hadithi ya Ibnu Abbass (r).
(8) Asbab al-Nuzool, by al-Wahidi, on the authority of Ibn Abbas
(9)Al- Musnad ya Imam Ahmad Ibn Hanbal, jalada la 5, uk. wa 38
Amma Thaalabi alipofika kwenye Sura 5:55-56 amenakili maelezo ya hadithi yenye simulizi za Sahaba Abu Dhar al Ghifari ( r.a ) kuwa amesema: "Masikio yangu yote mawili yawe hayasikii tena na macho yangu mawili yapofulewe kama ninasema uongo, nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani ziwe kwake akisema, "Ali ni Kiongozi wa wachamungu na ni Muwaji wa makafiri, atakayemsaidia atakuwa mshindi pamoja naye na atakayemwacha naye ataachwa". Siku moja niliswali na Mtume Muhammad (s), masikini akaja kwa ajili ya sadaka, lakini hapakuwa na ye yote aliyempa sadaka hiyo, wakati huo huo Ali alikuwa katika hali ya kurukuu na akamuashiria masikini huyo kuchukuwa pete yake kwenye kidole chake, hapo Mtukufu Mtume akamtukuza Allah na kusema "Allahu Akkbar"! Kaka yangu Mussa (a.s) alikuomba akisema ewe mola wangu, ukunjuwe moyo wangu kwa kuifanya kazi yangu nyepesi na niondolee utata uliopo kwenye ulimi wangu ili waweze kunifahamu, na mchague kutoka miongoni mwa ahli zangu Harun ambaye ni ndugu yangu awe waziri wangu na nitie nguvu kwa ajili yake na mfanye ashiriki kwenye kazi yangu ili tuweze kukutukuza na kukukumbuka wewe kila mara.
Kwa hakika unatuona.' Na ewe Mola wangu ukamwambia Mussa kuwa, ewe Mussa, nimekutakabalia maombi yako, ewe Allah! Mimi ni mja wako na Mtume wako. Ung’arishe moyo wangu pia na nifanyie kazi yangu iwe nyepesi na mfanye Ali ambaye ni miongoni mwa ahli zangu kuwa waziri wangu na mfanye yeye awe ni nguvu kwangu". Kisha Abu Dhar akaendelea kusema; Wallahi! Mtume hakumaliza dua yake isipokuwa Siddiq Jibriil alishuka na aya hii "INNA-MA WALIYYUKUM ALLAH .... (Sura ya 5 aya ya 55-56): "Hakika Allah ndiye Msimamizi wa mambo yenu, na Mtume wake pia na wale walioamini ambao wanasimamisha Swala na kutowa Sadaka hali wao wanarukuu. Na ye yote atakayemfanya Allah na Mtume wake na wale walioamini kuwa ndio wasimamizi wa mambo yake, hakika kundi la Allah ndilo litakalofaulu"
Tafsir al-Kabir, ya Imam al-Tha'labi
chini ya maelezo ya Sura 5:55-56. Mawahhabi,
jee Imam Thaalabi hakujua ipi hadithi Sahihi na ipi hadithi Dhaifu, na kwamba
wewe unajuwa zaidi zipi Hadithi sahihi na zile zisizokuwa Sahihi?
Comments
Post a Comment