UTUME

Mwenyezi Mungu anasema yafuatayo kuhusu Utume:
  
“Na hatuwatumi wajumbe (Mitume) isipokuwa ni wenye kutoa bishara na wenye kuonya, kwa hivyo basi Mwenye kuamini na akatenda mema (watu hao) hakuna khofu juu yao na wala hawata huzunika”.

“Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu kilicho teremshwa kwa mtume wake na Kitabu kilicho teremshwa kabla yake. Na mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake, na siku ya mwisho, hakika amepotea upotovu ulio mbali (na haki).

“Na Mwenyezi Mungu aliwatumia Mitume mmoja baada ya mwingine ili wawakumbushe ahadi (agano) ya maumbile yake (iliyoko kwenye maumbile), na wawakumbushe neema zake zilizo sahaulika, na wawatolee hoja kwa kuwafikishia ujumbe, na wawafunulie mambo yaliyo fichwa akilini mwao (ili wazitumie ipasavyo)”.  Mtume wa mwisho wa Umma huu ni Nabii Muhammad (s.a.w.w) nay eye ndiye nuru ya uongozi kwa wanadamu wote.

“ufafanuzi huo ni kwa mujibu wa Amirul-muuminin ALi bin Abi-twaalib (a.s)”.

Comments