BAHLUL AMSHAURI KHALIFA HARUN RASHID

BAHLUL AMSHAURI KHALIFA HARUN RASHID:
Siku moja Bahlul alimtembelea Harun al-Rashid, na aliombwa atoe nasiha.
Hapo Bahlul alianza: "Ewe Harun! Iwapo wewe utakuwapo porini ukashikwa na kiu ya maji ambayo hayapatikani, huku ukikaribia kufa. Je utalipa pesa kiasi gani kwa kiasi cha kikombe kimoja cha maji?"
"Sarafu za dhahabu (Dinar)!" alijibu Harun.

"Iwapo mwenye maji asiporidhia sarafu hizo, je utampa nini badala yake?" aliendelea kusema Bahlul.
"Nitampatia nusu ya ukhalifa wangu" alikatiza Harun kwa haraka.

"Naam, baada ya kumalizia kiu chako, ukashindwa kupata mkojo (ukaziba) nawe usiweze kujitibu, je utampa nini yule atakaye kutibu huo ugonjwa?" Aliuliza Bahlul.
"Nitampatia sehemu ya nusu ya dola yangu iliyobakia "Harun akanena katika hali ya bumbuwazi.

Basi hapo kwa kupumua, Bahlul alisema: "Ewe Harun! Usijivunie Ukhalifa wako ambao unajua uthamani wake ni sawa na kikombe cha maji na uponyaji wa ugonwa wako. Hivyo, ni kheri yako iwapo utawatendea watu wako kwa upole na haki!"
MAZINGATIO
Tawala zilizofuatia baada ya Mtume (s.a.w.w) kufariki, hazikutenda haki kwa waislamu na wanadamu wengine kama ilivyokusudiwa na Uislamu isipokuwa utawala wa Imam Ally (a.s) uliodumu kwa miaka minne ya misukosuko, kwani waliozoea kufisidi hawakuweza kumwachia imam aongoze kwa amani. Hivyo walimshambulia kutoka kila kona mpaka walipomuua akiwa anaswali msikitini.

Nadhani utakumbuka kuwa Abubakar aliposhika utawala tu aliwauwa waislamu waliogoma kulipa zaka kwa sababu ya kushangazwa na taarifa za kwamba khalifa ni Abubakar badala ya Imam Ally (as). Abubakar badala ya kuwaelimisha, alimwagiza Khalid bin Walid aongoze jeshi kwenda kuwachinja. Waliuawa wote. Khalid bin Walid akambaka mke wa Malik pembeni tu na maiti yake. Huu ni msiba mkubwa kuwakuta waislamu.


Hii ndio sasa Bahlul anamwambia khalifa asijivunie ukhalifa bali awatendee wema watu wake. 

Comments