BAHLUL KUKALIA KITI CHA KHALIFA

Siku moja Bahlul aliingia katika Qasri ya Khalifa na kukuta kiti chake ki tupu aliona hakuna mtu wa kumzuia, hivyo alikwenda moja kwa moja akaketi juu ya kiti cha Khalifa.
Walipotokezea maaskari wa Khalifa, walijaribu kumwondoa Bahlul, lakini alikataa, hivyo waliweza kumwondoa kwa kumpiga. Hapo Bahlul alianza kulia kwa sauti, na alipotokea Harun Rashid alimwona Bahlul akilia kwa sauti na aliwauliza maaskari wake sababu. Wao walimwelezea yote yaliyotokea. Hapo Khalifa aliwakemea maaskari hao na kumpa pole Bahlul.
Kwa hayo, Bahlul alisema: "Mimi sikililii kile kilichonipata, bali ninakulilia wewe Khalifa, kwani mimi nimeteswa kwa kuketi punde tu, je wewe utateswaje kwa kukikalia kiti hiki kwa miaka yote hiyo kwani kiti hiki cha Ukhalifa ni kwa ajili ya watu wengine na wewe
umewadhulumu hao, na kukikalia kwa mabavu!"


MAFUNDISHO:
Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliache ameteua Imam Ally (a.s) kuwa khalifa, afuatiwe na Imam Hassan kisha Imam Hussein (a.s) na jumla ya maimamu ni 12 wote ni Bani Hashim na wote ni Ahlulbayt wa Mtume (s.a.w.w), lakini Mtume alipokufa wababe wakakimbilia katika ukumbi ya Saqifa na kuchaguana kwa mabavu, na huo ukawa mwanzo wa matezo na Madhila kwa Ahlulbayt na ikafungua njia kwa madhalimu kupora madaraka na kujiita kuwa makhalifa. Hiyo ndio anayoiongelea Bahlul katika kisa hiki. Hivyo tuwe upande wa Mtume na Ahlulbayt wake kama kweli tunataka kheri ya dunia na akhera, lakini kama tunataka sifa za dunia pekee basi tuendelee kuwa maadui wa Mtume na Ahlulbayt wake (a.s).

Comments