BANI UMAYYA NA UTIAJI NAJISI WA MAKUBURI YA MASAHABA

Kwa mfano, alipouawa shahidi Zaid bin Ali bin Husein, ajulikanaye kama Zaid Shahid, na kuuwawa shahidi kwa mtoto wake, Yahya. Wanahistoria wote wa Shi’a na Sunni wameandika kwamba wakati
Hisham bin Malik alipokuwa Khalifa, alitenda maovu mengi. Mwishowe, Zaid bin Ali, mtoto wa Imamu Zainu’l-Abidin na anayejulikana sana kama mwanachuo mkubwa na mwanatheolojia mchamungu, alikwenda kumuona Khalifa kutafuta haki kwa ajili ya manung’uniko ya Bani Hashim (Kumbuka tokea kifo cha Mtume, familia yake iliteswa kila kukicha).

Lakini punde tu Zaid alipowasili, Khalifa badala ya kumsalimu kama mtoto wa moja kwa moja wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alimtukana kwa lugha ya kuchukiza sana ambayo siwezi kuirudia hapa.
Kwa sababu ya kudhalilishwa huku alikofanyiwa, Zaid aliondoka Syria na kwenda Kufa, ambako aliunda jeshi dhidi ya Bani Umayya. Gavana wa Kufa, Yusuf bin Umar Thaqafi, alitoka na jeshi kubwa kumkabili. Zaid alisoma shairi lifuatalo: “Maisha ya udhalilifu na kifo cha heshima, vyote ni chembe zenye uchungu, lakini kama moja wapo lazima ichaguliwe, chaguo langu ni kifo cha heshima.”
Ingawa alipigana kishujaa, Zaid aliuwawa katika mapigano hayo. Mtoto wake, Yahya, alichukua mwili wake kutoka kwenye uwanja wa vita na akamzika mbali kutoka mjini karibu na ukingo wa mto, na kusabibisha maji kupita juu yake. Hata hivyo, kaburi hilo
liligunduliwa, na chini ya amri ya Yusuf mwili huo ulifukuliwa, kichwa cha Zaid kilikatwa na kupelekwa Syria kwa Hisham.

Katika mwezi wa Safar, 121 A.H., Hisham aliamuru mwili mtakatifu wa mtoto huyu wa Mtume (s.a.w.w) uwekwe kwenye kiunzi cha kunyongea (msalaba) ukiwa uchi kabisa. Kwa muda wa miaka minne ulikaa kwenye kiunzi cha kunyongea.

Baadae, wakati Walid bin Yazid bin Abdu’l-Malik bin Marwan alipokuwa Khalifa katika mwaka wa 126 A.H., aliamrisha kwamba mifupa ile itolewe kutoka kwenye kiunzi cha kunyongea, ichomwe, na jivu lake lisambazwe juu lichukuliwe na upepo.

Mtu huyu aliyelaaniwa alitenda uovu kama huu huu kwenye mwili wa Yahya bin Zaid. Mtu huyu mtukufu vile vile alipinga uonevu wa Bani Umayya. Yeye pia aliuwawa katika medani ya vita. Kichwa chake kilipelekwa Syria na kama alivyofanyiwa mtukufu baba
yake, mwili wake ulitundikwa kwenye kiunzi cha kunyongea kwa muda wa miaka sita.

Marafiki na maadui wote kwa pamoja walilia walipouona mwili wake. Waliu’d-Din Abu Muslim Khorasani, ambaye alipigana dhidi ya Bani Umayya kwa niaba ya Bani Abbas, aliuchukuwa mwili wake na kuuzika huko Gurgan.
Ngugu wanadamu wenzangu, huu ndio unyama wa bani Umayya ambao unaendelezwa leo na mawahhabi kwa madai yale yale ya kwamba wanautetea Uislamu. Hii ni misiba miwili kwa pamoja. Mauaji wayafanyayo ni msiba, lakini kudai kuwa wao ni waislamu ni msiba mkubwa zaidi kwa sababu tabia zao sio za kiislamu na hivyo huishia kuudhalilisha Uislamu.

Ebu jiulize Mtu anauteteaje Uislamu kwa kuua familia ya Mtume (s.a.w.w) ambao nao ni waislamu kama wao na hata huenda ni waislamu bora zaidi kwa sababu wao wanaujua zaidi Uislamu kwa sababu ni wao ndio walioishi kwa muda mwingi na Mtume na kufundishwa zaidi. 

Comments