FAIDA YA SWAUMU KIROHO

Tunaelewa vizuri kwamba makusudi ya kuumbwa kwetu ni kutupatia kufikia ukamilifu wa roho. Na kwa ajili ya kutimiza makusudi hiyo roho kuelekea upande wa juu kiutakatifu; vile vile inapasa roho iangalie utaratibu na usalama wa kiwiliwili. Anapokuwa mtu yu macho, tena mandhali tumbo lake limejaa, basi roho haijaliwi kupata wasaa kuelekea upande wa Mola kwa vile umeshughulika na mambo ya mwili; inaziwika kuipata shabaha ya kuumbiwa kwake.

Kwa hivyo mtu akifunga mchana kiwiliwili kinakuwa chepesi, na tukifanya mazowea usiku pia tule chakula chepesi na kiasi cha dharura tu, hapo roho itapata wasaa na faragha kwa upesi. Ijapokuwa kwa muda huo mdogo wa mwezi mmoja mfululizo bila ya taabu itaweza kushikamana uhusiano wake wa juu kwa furaha na kupata daraja tukufu za akhera.


Uvivu unapopungua itumie fursa hii kufanya ibada mbali mbali, kama vile kuswali na kutoa sadaka. Ibada hizi zina faida kubwa kwa mwanadamu na zitapelekea kuwa kipenzi wa Mwenyezi Mungu. Malipo yake ni makubwa kiasi kwamba ni Allah peke yake ndiye anayefahamu. 

Comments