Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), “Mwenyezi Mungu hakumtuma Mtume yeyote wala hakumpa ukhalifa Khalifa yeyote isipokuwa anakuwa na makundi mawili, kundi moja linamuamrisha kutenda mema na kumhimiza juu ya hayo mema, na kundi jingine linamuamrisha kufanya mambo ya shari na kumsisitiza juu ya shari hiyo, basi Maasum ni Yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu.
Rejea
o Sahihi Bukhari, Juzu ya 4 ukurasa wa 173
o Musnad Imam Ahmad, Juzu ya 3 ukurasa wa 39
Hadith hii inaonesha dalili ya wazi kuwa masahaba walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili yaani walikuwepo Masahaba waliokuwa wakimsaidia na kumhimiza Mtume katika mema aliyokuwa akiyaongoza Mtume wetu. Lakini kuna kundi jingine la Masahaba ambalo lilijikita katika kazi ya kumshawishi Mtume kufanya maovu na kutumia juhudi zao zote kuzuia mema aliyokuwa ametuletea Mtume wetu.
Kundi hili la pili lilikuwa likipinga kila alichokuwa akikiagiza Mtume na wapambe wao walizua hadith mbalimbali ya kuwa watu hao wanapompinga Mtume, Allah huleta aya kukubaliana na lai za watu hao waliokuwa wakijaribu kumpotosha Mtume.
Kwa mfano Mtume alimteua Imam Ally (a.s) awe khalifa baada ya yeye Mtume kufariki dunia. Lakini kundi hilo la pili lilifanya juhudi kubwa kuzuia Uongozi wa Imam Ally na utakuta tarekh inanukuu watu hao walikuwa wakimchukia sana Imam Ally na kufanya kampeni ili watu wamchukie.
Kundi hilo la pili liliposikia kuwa Mtume amefariki dunia, kwanza waliwazuia watu wasitangaze msiba huo, kisha walikusanyika katika ukumbi uitwao Saqifatu bani Saidah na kufanya uchaguzi, kinyume na maelekezo na Sunnah ya Mtume wetu. Tokea lini Uislamu ukaamrisha watu wafanye uchaguzi? Wakafanya uchaguzi bila tume ya uchaguzi, tena hakuna sheria za uchaguzi, na watu waliohudhuria hawakualikwa kwa utaratibu ulioeleweka kwa wengi na hivyo waliohudhuria ni kile kikundi cha waliokuwa wakiamrisha maovu kitupu na hatimaye waliofanya uchaguzi ni watu wachache tu miongoni mwa watu wa Madina. Lakini wafuasi wao utawakuta mpaka leo wanapinga uchaguzi na kujifanya kuwa wamesahau kuwa Masahaba wanaowafuata wao walikwenda kufanya uchaguzi, na kuiacha maiti ya Mtume ndani na wala hawakushiriki katika mazishi ya Mtume wetu.
Hivyo ninakuombeni ndugu zanguni katika imani rudini katika Uislamu sahihi nao ni kufuata lile kundi la Masahaba ambao walikuwa wakimhimiza Mtume kutenda mema na wakaafikiana na maelekezo yote ya Mtume na kuachana na masahaba waliokuwa wakipingana na Mtume katika maelekezo yake.
Mfano wa kikundi cha kuamrisha maovu umenukuliwa na Tarekh Baghdad Juz. 1 uk. 133 hivi, “Kuna watu miongoni mwa Makuraishi walikuja kwa Mtume wakasema, ewe Muhammad bila shaka sisi ni jirani zako na tumewekeana nawe ahadi, na kwa hakika kuna watu katika vijana wetu wamekujia wewe, wala hawana haja na Uislamu wala kutaka kujifunza, bali hakuna lolote ila wamekimbia kutoka katika miliki zetu. Mtume akamuuliza Abubakar, wasemaje? Akasema, wasemavyo ni kweli, wao ni jirani zako na umewekeana nao ahadi. Uso wa Mtume ukabadilika kwa maelezo aliyoyatoa Abubakar. Kisha Mtume akamuuliza Umar bin Khatab, wasemaje? Umar naye akasema, wasemavyo ni kweli, hakika wao ni jirani zako na umewekeana nao ahadi. Basi uso wa Mtume ulibadilika zaidi kwa maelezo aliyoyatoa Umar.
Utaona kuwa Masahaba hawa wawili waliungana na washirikina kuwashutumu waislamu wenzao kuwa hawakusilimu kwa kuufuata Uislamu bali wanamalengo mengine tu. Kama Mtume angekubaliana nao ingetokea kitu kinachotokea sasa ambapo baadhi ya watu wanaodai kuwa ni waislamu huwashutumu waislamu wenzao na kuwaita kuwa ni watu wa bid’a, makafiri na huwahukumu kifo. Haya ndio matunda ya kuwafuata Masahaba hao waliokuwa wakimuamrisha Mtume kufanya yaliyokuwa ya shari. Kazi ya waislamu hawa imekuwa kuamrisha utengano baina ya waislamu na wamewafanya waislamu wenzao kuwa ndio maadui zao badala ya wayahudi na washirikina kama tulivyoagizwa na Allah.

Comments
Post a Comment