Amesema Mtume Mohammad (S.A.W.W), “Mimi ni mwenye kukutangulieni na ni shahidi juu yenu, na bila shaka mimi namuapa Mwenyezi Mungu, nakiangalia kidimbwi changu sasa hivi na kwa hakika nimepewa funguo za hazina ya ardhi nami namuapa Mwenyezi Mungu, sihofii kwenu kwamba mtafanya ushirikina baada yangu, lakini ninawahofia kuwa mtashindania Ulimwengu.
Tazama: Sahihi Bukhari Juzu ya 4 ukurasa wa 100 – 101.
Amesema kweli Mtume wetu kwani Masahaba waliigombania dunia mpaka wakazichomoa panga zao kupigana wao kwa wao na kukufurishana. Na baadhi yao walikuwa mashuhuri kwa kukusanya dhahabu na fedha wakati waislamu wengine wakifa njaa. Wanahistoria kama vile Al-Masudi ndani Muroojud-Dhahabi (juz. 2 uk. 341) na Tabari wanatusimulia kwamba utajiri wa Zuberi peke yake ulifikia dinari elfu hamsini na farasi elfu moja, watumwa elfu moja na ardhi kubwa katika miji ya Basra, Kufah, Misri na maeneo mengine.
Ukisoma rejea hiyo hiyo utakuta kuwa Abdurahman bin Auf alikuwa na farasi 100, ngamia 1,000, mbuzi 10,000. Naye Uthuman bin Afan siku aliyokufa aliacha dinari 150,000 ukitoa ardhi na mifugo. Ama Zaid ibn Thabit aliacha dhahabu na fedha ambazo zilikuwa zikivunjwa kwa mashoka mpaka mikono ya watu ikawa na malengelenge.
Hii ni baadhi ya mifano michache ya Masahaba waliokuwa wakijilimbikizia mali kwa namna zote halali na haramu cha msingi tu wapate mali.

Comments
Post a Comment