Uislamu una mfumo mzuri wa ndoa na
haki za wanawake, kinyume na wanavyoamini watu wa Magharibi na wengine
waliokuwa na kasumba ya umagharibi.
Inakubaliwa na kila rafiki na adui
kuwa Qur.ani Tukufu ilifufua haki za wanawake. Hata maadui wanakiri angalau
kwamba Qur’ani wakati wa kuteremshwa kwake ilichukuwa hatua kubwa katika
kuboresha hali ya mwanamke na kurejesha haki zake za binadamu.
Qur.ani ilifufua haki za mwanamke
kama mwanadamu na kama mwenzi wa mwanaume katika utu na haki za binadamu lakini
haikupuuza jinsia yake wala jinsia ya mwanaume. Kwa maneno mengine Qur.ani
haikupuuza maumbile ya mwanamke.
Ndio maana kuna kuwafikiana
kikamilifu kati ya kanuni za
maumbile na kanuni za Qur.ani.
Mwanamke katika Qur.ani ni sawa na mwanaume katika maumbile. Vitabu hivi viwili
vikubwa vya kimungu (Qur.ani na maumbile), kimoja kikiwa kimeumbwa na kingine
kikiwa kimekusanywa, vinakubaliana na kuafikiana kabisa. Nia ya kitabu hiki ni kuangazia
na kuelezea kuafikiana huku.
Kutokana na umuhimu wa maudhui hii
nitaendelea kutoa makala katika maudhui hii kwa sababu makala hizi
zitawanufaisha wengi, waislamu na wasio kuwa waislamu.
Comments
Post a Comment