HEDHI NA NIFASI (mafunzo kwa akina mama)

Hedhi ni damu inayomtoka mwanamke katika utupu wa mbele, aliyefikia miaka tisa. Na mwisho wa kutoka kwa damu ni miaka hamsini.
Inazuiwa kwa mwenye hedhi mambo yafuatayo:
(a) Kushika Qur-an, (b) Kukaa Msikitini, (c) Kuswali, (d) Kufunga saumu, (e) Kumwingilia, (f) Kumwacha (kumpa talaka).
Muda wa hedhi ni siku tatu kwa desturi, na wingi wake ni siku kumi. Mwenye hedhi baada ya kutoharika anapaswa kulipa funga na wala hatalipa swala. Nifasi ni, damu ambayo hutemwa na mfuko wa uzazi kwa sababu ya kuzaa. Kwa hiyo, mwenye mimba akizaa na kusitoke damu, basi hakuna josho, muda wa nifasi ni siku kumi.
Inazuiwa kwa mwenye nifasi mambo yaleyale yanayomzuia mwenye hedhi. Je, vitabu vya wakristo vinasema nini katika rnada hii? Na tusome;
"Mwanamke yeyote anapokuwa mwezini, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba. Mtu yeyote atakayemgusa mwanamke huyo atakuwa najisi mpaka jioni. Kitu chochote anacholalia au kukalia wakati yu najisi kitakuwa najisi. Mtu yeyote atakayegusa Kitanda cha huyo mwanamke ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni." Mambo ya Walawi 15:19-22.

Ukristo unamnyanyapaa mwanamke katika siku saba anazokuwemo katika hedhi. Lakini, si yeye peke yake bali kila mtu sasa anayegusa chochote kilichoguswa na mwanamke huyo, naye huwa najisi, inamlazimu kufua mavazi yake na kuoga, hata hivyo huendelea kuwa najisi mpaka jioni'

Comments