BABA ZAKE WADOGO.
Mtume (s.a.w) ana baba wadogo tisa (9), nao ni watoto
wa Abdul Mutwalib kama wafuatao: 1- Al Haarith. 2- Zubair. 3-
Abu Twalib. 4- Hamza. 5- Al Ghidaaq, 6- Dharaar Al muqawwim, 7- Abu Lahab.
8- Al Abbas.
SHANGAZI ZAKE MTUME (S.AW).
Mtume (s.a.w) alikuwa na shangazi sita kutokana na akina mama
tofauti nao ni kama wafuatao: 1- Umaimah. 2- Ummu Hakiimah. 3-
Burrah. 4- Aatikah. 5- Swafiyyah. 6- Arwy.
MAWASII WAKE MTUME (S.A.W).
Mawasii wake ni kumi na mbili, nao ni kama wafuatao: 1- Amirul
muuminnina Ally bin Abii twalib (a.s). 2- Hassan bin Ally
(a.s) 3- Hussein bin Ally (a.s) 4- Ally bin Hussein (a.s). 5-
Mohammad bin Ally ( a.s) 6- Jaafar bin Mohammad (a.s) 7- Mussa bin
Jaafar (a.s) 8- Ally bin Mussa (a.s) 9- Mohammad bin
Ally (a.s) 10- Ally bin Mohammad (a.s) 11- Hassan bin
Ally (a.s) 12- Al Hujjat binil Hassan (Mohammad Mahdii
) (a.s).
MLINZI WAKE.
Mlinzi wake alikuwa ni Anas.
WAIMBAJI MASHAIRI WA MTUME (S.A.W).
1 – Hassan bin Thabiti. 2- Abdallah bin Rawaha. 3-
Kaab bin Maalik.
WAADHINI WA MTUME (S.A.W).
1- Bilal Al –Habashi 2- Ibnu Ummu
Makhtuum. 3- Saad Al-Qurt.
NEMBO YA PETE YA MTUME (S.A.W).
Nembo ya pete yake ilikuwa ni (( Mohammad Rasuulu
llah)).
UMRI WAKE (S.A.W).
Ali ishi kwa muda wa miaka 63.
MUDA WA UTUME WAKE (S.A.W).
Utume wake ulidumu kwa muda wa miaka 23.
TAREHE YA KUFARIKI KWAKE (S.A.W).
Alifariki dunia tarehe 28 mwezi wa safar mwaka wa 11
hijiria.
SEHEMU ALIYO FIA (S.A.W).
Mtume alifia katika mji wa Madinatul Munawwarah.
SEHEMU ALIYO ZIKIWA (S.A.W).
Alizikiwa katika mji wa madina ndani ya nyumba yake tukufu.
Kwa ufafanuzi zaidi rejea katika kitabu Buharul
an’waar juzuu ya 15-16,kwa wale wenye kufahamu lugha ya kiarabu.
Comments
Post a Comment