Kitu kimoja kinaweza kuwa na madhara mengi, lakini kikawa na faida japo kidogo. Mfano mzuri ni ulevi na kamari, Quran tukufu inajibu wazi wazi swali aliloulizwa Mtume s.a.w: "Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari, waambie katika hayo mna uovu mkubwa na manufaa (kidogo) kwa watu, na uovu wake ni mkubwa zaidi kuliko manufaa yake." 2:219.
Ukimuuliza mvutaji tumbaku: Kwa nini unavuta? Atajibu: Inaniburudisha. Ingawa anafahamu vizuri madhara yake: "Wataalamu kadhaa wanahesabu kwamba, kuvuta tumbaku ni aina moja ya kujiua, hivyo, kujiua hakuruhusiwi katika dini au madhehebu yoyote."
Maoni au fatwa za wanavyuoni wa Kiislamu zinatofautiana kuhusu suala la uvutaji tumbaku. Wengine wameharamisha moja kwa moja, wengine wameharamisha kwa wale wanaotaka kuanza kuvuta, na wengine hawakutoa fatwa maalum kuhusu jambo hilo.
Wanavyuoni, wataalamu na hata wavutaji tumbaku wenyewe, wanakubaliana kwamba tumbaku hudhuru afya ya mtu. Kwa hivyo, inapasa kwa mzoefu wa tumbaku kuzingatia vipengele vyote hivyo, hasa kwa faida yake mwenyewe, na kwa jamii nzima kwa jumla.

Comments
Post a Comment