ITIKADI YA SHIA ITHNA
ASHARIA KUHUSU KUWEPO KWA MOLA MTAKATIFU.
Sisi tunaamini kuwa
Mwenyeezi Mungu ndiye muumbaji wa vitu vyote, na athari ya utukufu na elimu
yake inaonekana kwa uwazi kabisa katika kila kiumbe ulimwenguni, katika umbile
la mwanaadamu, wanyama, mimea, katika nyota ziliopo mbinguni, na katika kila
kitu ulimwenguni.
Sisi tuna itikadi ya
kuwa; kila tukifikiri na kutafakuri zaidi kuhusiana na siri ya viumbe vyote
duniani, tutafahamu utukufu wa elimu na qudra ya dhati ya Mola Mtakatifu, na
kwa kuonekana maendeleo ya elimu na taaluma ya wanaadamu ya kila siku
kunapatikana na kufunguka elimu mpya kutokana na elimu na hekima zake Allah
(s.w), na tafakuri za wanaadamu zinazidi kukua na kuenea kwa wingi zaidi, na
tafakuri hizo ndio chanzo cha kuwa karibu naye Mola mtakatifu na kunufaika na
upeo wa nuru ya utukufu wake. Qur-ani takatifu inasema:-
Na katika ardhi zipo
Ishara kwa wenye yakini. Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?.2
Hakika katika kuumbwa
mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. Ambao
humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na
hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi
bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.3
Mola wetu Mlezi! Hakika
sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi;
nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na
utufishe pamoja na watu wema.1
REJEA:
[1] Surat Al-Imrani
Aya ya 193
[2] Surat
Adh-Dhariyat Aya ya 20-21
[3] Surat al-Imrani
Aya ya 190-191
Comments
Post a Comment