JE, INAWEZEKANA KUWA MLANGO WA IJTIHADI UMEFUNGWA?

Masunni wamejitia katika uziwi kwa kudai kuwa mlango wa Ijtihad umefungwa na kwamba siku hizi hawezi kupatikana Mujtahid, lakini kuna mambo mengi yanayohitajia uchunguzi lakini wanaogopa kufanya hivyo kwa kuogopa dhambi ya kufanya ijtihad. Je, ni nani aliufunga mlango huu wa ijtihad? Je ni kweli kuwa maimamu Abunifa, Maliki, shafii na Hanafi walikuwa na ubora wa kutushinda sisi kiasi cha wao kuruhusiwa kuwa mujtahid lakini sisi tusiruhuwe? Na ni nani aliwapa mamlaka hayo ya kuwa mujtahid na wasemaji wa waislamu?

Ikiwa Muawiyah aliwauwa watu wasiokuwa na hatia na kuwavunjia heshima, nanyi mnasema kwamba alijitahidi akakosea na atapata ujira mmoja. Na iwapo Yazid ndiye aliyewaua watoto wa Mtume katika eneo linaloitwa Karbala na akaruhusu jeshi lake liukalie mji wa Madina na kuwadhalilisha wakazi wake na bado ninyi mnasema kuwa alifanya ijtihadi akakosea atapata ujira mmoja, kiasi kwamba baadhi yenu wamesema kuwa, “Imam Hussein (a.s) aliuawa kwa upanga wa Babu yake,” ili walitakase tendo hilo baya. Imefikia mahali mkampongeza Khalifa Abubakar kwa kuwauwa watu waliogoma kulipa zaka kipindi cha utawala wake na huku mkijua kuwa Mtume hakuwauwa watu waliogoma kutoa zaka.


Kwa nini sasa mnawatisha watu pale wanapofanya uchunguzi wa mambo yaliyotokea baada ya Mtume kufa? Mtu akisema kuwa Abubakar alipora madaraka ya Imam Ally (a.s) kwa nini mnakimbilia kumtukana kuwa ni kafiri badala ya kusema amefanya ijtihadi na kukosea hivyo atapata ujira mmoja? Na sisi watafiti tunaposema maovu ya Masahaba hatukusudii kuwadhalilisha bali ni utafiti tu. Ijitihad hii bila shaka Mwenyezi Mungu atatulipa ujira mmoja kama ambavyo atawalipa ujira mmoja akina Abubakar, Umar, Uthuman, Muawiyah na Yazid.

Comments