JE MITUME HAWARITHIWI?

Swali hili walijibu wale watu wanaobariki dhulma aliofanyiwa bi Fatumah (a.s) kwa kunyimwa mirathi ya baba yake yaani Mtume Mohammad (S.A.W.W). Abubakar alipofuatwa na bibi huyo mtukufu na kuombwa ampe haki yake ya Mirathi, alitoa hadith ya uongo kuwa mitume hawarithiwi. Japokuwa Bi Fatumah (a.s) alitoa ushahidi wa aya kuwa kila mtu anarithiwa na kwa kuwa Mtume alikuwa mtu naye anarithiwa lakini bado Abubakar aling’ang’ania kuwa mitume hawarithiwi. (Kumbuka hadith haiwezi kufuta aya).
Kama madai ya Abubakar ni ya kweli, mbona kuna riwaya zinazoonesha kuwa kuna watu walimrithi Mtume wetu na wapo wengine pia waliendelea kudai mirathi yao baada ya Abubakar kufariki.
Ibn Abasi alimwambia bibi Aisha katika beti zifuatazo, “Ulipanda ngamia, ukapanda nyumbu, lau utaishi zaidi utapanda tembo, wewe unayo sehemu moja kati ya tisa lakini thumuni yote umeitumia peke yako.
Maneno haya ya ibn Abasi yanaonesha kuwa bibi Aisha alichukuwa urithi wote uliostahili kuchukuliwa na wanawake walioachwa na Mtume pindi alipofariki dunia. Je, huu ndio uislamu na ubora wa mama huyu wa waumini?
Ibn Abil Hadid Al-Muutazili amesema ndani ya sharh ya Nahjul Balagha kuwa, “Mabibi Aisha na Hafsa walimwendea Uthman bin Afan katika zama za ukhalifa wake, wakamtaka awagawie urithi wao kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w). Uthuman alikuwa kajiegemeza akakaa sawa na kumwambia Bibi Aisha, “Wewe na huyu mwanamke aliyeketi mmemleta bedui ambaye hujitahirisha kwa mkojo wake na hali ya kuwa ninyi mnashuhudia kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kasema, ‘sisi Mitume haturithiwi’, ikiwa kweli Mtume harithiwi, basi ninyi mnataka nini baada ya hayo? Na iwapo Mtume anarithiwa ni kwanini basi mlimnyima Fatuma haki yake? Bibi Aisha akaondoka mbele ya macho ya Uthuman hali ya kuwa amekasirika na akasema, “Muuweni Naathal, hakika amekufuru”. Hivyo bi Aisha anamchango katika kifo cha Uthuman bin Afan kwa kosa la kumnyima mirathi iliyotokana na kudhulumiwa Fatumah si mirathi tu bali hata mali zake binafsi ziliporwa.
Soma:
Sharh Nahjul Balagha cha ibn Abil Hadid, juz. 16 uk. 220 – 223.

Comments