kaburi
la Amiru’l-Mu’minin ‘Ali (as) liligunduliwa miaka 150 baada ya kifo chake
kutokana na kufichwa na Ahlulbayt (a.s) ili maadui wa Mtume na Ahlulbayt
isijekujua alipozikwa na hivyo kulidhihaki kaburi hilo na hata kumfukua na
kumuwamba msalabani.
Uonevu
wa Banu Umayya ulikuwa mkali sana wakati wa mwisho
wa
uhai wa ‘Ali, hivyo aliagiza katika wosia wake kwamba azikwe kwa siri wakati wa
usiku, na kwamba isiachwe alama yoyote ya kaburi hilo.
Ni
jamaa zake wachache tu wa karibu na watoto wake ndio waliohudhuria mazishi
yake. Asubuhi ya tarehe 21 Ramadhan siku ambayo ilikuwa ndio azikwe, misafara
miwili ilitayarishwa. Mmoja ulielekezwa kwenda Makka, na mwingine kwenda
Madina.
Hii
ndio sababu iliyofanya kwa miaka mingi kaburi lake lisijulikane, isipokuwa kwa
jamaa zake wachache na watoto wake tu. Na wengi wa Masunni waliamini kuwa
jeneza la imam Ally (a.s) lilipaa kwenda mbinguni kutokana na kukosa kwao kujua
imam alizikwa wapi.
Mwenendo
wa Banu Umayya uliokuwa sio wa kidini, Walikuwa maadui makhususi wa jamaa ya
kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Wangeweza kulivunjia heshima kaburi lake. Subuhana-LLAH!
Maovu yalioje waliyoyafanya! Damu iliyoje waliyoimwaga, na heshima zilizoje
walizozivunja!
Kwa
aibu kubwa, wanachuoni wa kisunni wakubwa wameandika jinai zao nyingi. Allama
Maqrizi Abu’l-Abbas Ahmad bin Ali Shafi’i ameandika maovu ya Banu Umayya
yanayoumiza moyo kabisa katika kitabu chake Annaza’ Wa’t-takhasum
fima baina Bani Hashim wa Bani Umayya.
Hakika kimeweka wazi
maovu makubwa sana kwa mfano mwaka wa pili wa utawala wa Yazid bin Muawiyya (khalifa
wa kiwahabi) waliuteka mji wa Makkah na kuwa waislamu elfu saba na kuwabaka
wanawake elfu tatu tena kwa amri ya khalifa huyu wa Mawahhabi pale alipowaambia
kuwa kila kitu ndani ya mji wa Maka ni halali kwao yaani wafanye watakavyo.
Comments
Post a Comment