JITAHADHALI AU WAOGOPE TAKFIR

Nimeonelea niandae mada kwa ajili ya kuuelimisha Umma wa Kiislamu katika Afrika Mashariki kuhusu kundi balaa ninaloitwa takfir. Takfir ni msamiati ambao unawakilisha makundi yote yanayojidai kuwa ni ya kiislamu na huku kazi yao ni kuwakufurisha waislamu wenzao na kuhalalisha mauaji dhidi yao.
Takfir wameendesha matukio ya kigaidi maeneo mengi duniani kwa kisingizio cha kwamba hao wanaowauwa ni makafiri au washirikina. Kutokana na uvivu wa kusoma wa watu hawa wamekuwa wakimwona mtu akifanya jambo lolote wasiololizoea basi humwita mtu huyo kafiri na kuhalalisha kumuua mtu huyo mara moja.
Hii imenisababisha nimkumbuke mwalimu wangu wa Sociology wakati nilipokuwa chuoni ambaye aliwahi kutuambia kuwa ukimwona mtu akimdhalau mtu mwingine elewa wazi mtu huyo anayemdhalau mwenzake hakusoma tamaduni za wenzake. Hivyo kutokana na kukosa kwake maarifa anaamua kumdhalau na kumdhalilisha mwenziwe. Lakini ukweli ni kuwa mtu huyo akipata wasaa wa kukaa na kujifunza utamaduni wa mdharauliwa atakuja kugundua kuwa yule aliyekuwa akimdhalau ni bora kuliko hata yeye mwenyewe.

Kwa hiyo asili ya utakifiri ni ujinga (murrakab) wa watu hawa ambao utawakuta wamekimbilia kufanya ibada lakini bila kutafuta elimu ya kile anachokiabudu ili akiabudu kwa ufasaha.
Ndipo wakipata hoja kutoka kwa mashia utawasikia wakisema, hao ni makafiri kwa sababu wanayo elimu kubwa sana lakini wanaitumia vibaya, kupotosha watu. Ukiwaambia twende ukajadiliane nao, hukataa kwa kuwa anayo yaamini hana yakini nayo wala ushahidi ya kuyathibitisha.
Ninahakika kuwa hayo niliyoyaandika yanatoka kuarifisha maana ya takfir na kwa msingi huu wasomaji wangu wamewaelewa takfiri wote na makundi yao hapa Afrika Mashariki. Labda kwa ufupi, ukimsikia mtu anamwita mtu mwingine kafir huyu basi elewa kuwa huyo ni takfir na yumo katika kundi potofu.

Imepokelewa na Kahhak kuwa Mtume wa Allah (s.a.w.w) alisema, “yeyote atakaye mlaani muumini, ni kana kwamba amemuua muumini huyo. Na yeyote atakaye msingizia muumini kuwa ni kafir, itakuwa kana kwamba amemuua pia”.
Hadith hii imepokelewa na Imam Bukhari na inaaminiwa na waislamu kuwa ni sahihi.

Abdullah bin Umar (r.a) alisema kuwa Mtume (s.a.w.w) alisema, “yeyote atakaye mwita ndugu ewe kafir, itakuwa mmoja wao ni kafir kweli.
Hadith zote hizo mbili zimepokelewa na Imams, Ahamad, Bazzar, Tabaraan, Baihaqi na kuandikwa katika vitabu: Majma’uz-Zawaa’id na Musnad Abu ‘Awaanah.


Mada hii itaendelea ili kuwaonya ndugu zangu waislamu na wajiepushe na kundi hili la shetani. Siwataji kwa majina kwa sababu wanaeleweka. Hata mada hii wakiisoma utakuta wananihukumu niuawe au kuniita kafir au yote mawili. 

Comments