KISA CHA KUADHIBIWA NA ALLAH WALIOPINGA UKHALIFA WA IMAM ALLY WALIADHIBIWA

KISA CHA KUADHIBIWA NA ALLAH WALIOPINGA UKHALIFA WA IMAM ALLY WALIADHIBIWA
Baada ya imam Ally (a.s) kutangazwa na Mtume (s.a.w.w) kuwa khalifa wake wa kwanza katika Hija ya kuaga na maeneo Ghadir Khum, kuna watu walijitokeza kulipinga hilo kama wanavyo fanya mawahhabi na masalafiya leo hii. baada ya kuenea kwa habari za Ghadir Khum na kusimikwa kwa Imam Ali kuwa ni Khalifa wa Waislamu kutokana na kauli ya Mtume alipowaambia "Aliyeshuhudia tukio hilo amfikishie habari asiyehudhuria ".
Habari hizo za tukio la Ghadir zilimfikia Harith bin Nuuman Al-Fihri na hakufurahishwa na habari hizo- Hapa kuna dalili kwamba walikuwepo watu waliodai kuwa ni Masahaba wakiishi Madina ambao walikuwa wakimchukia Ali na pia Mtume (s.a.w.w). Basi huyu bwana alimsimamisha mnyama wake mbele ya mlango wa msikiti akaingia kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: "Ewe Muhammad bila shaka wewe umetuamuru tushuhudie kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, tumekukubalia hilo, na umetuamuru tusali mara tano kwa siku, tufunge Ramadhan, Tuhiji na tutoe zaka mali zetu tukakukubalia, kisha hukuridhika kwa haya mpaka umeinyanyua mikono ya mwana wa ammi yako na umemboresha juu ya watu ukasema:
"Yeyote ambaye mimi ni mtawalia mambo yake basi Ali ni mtawalia mambo yake". Jambo hili latoka kwako au latoka kwa Mwenyezi Mungu"?
Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema hali ya kuwa macho yake yamekuwa mekundu: "Namuapa Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mola isipokuwa yeye, jambo hilo latoka kwa Mwenyezi Mungu na halitoki kwangu" Akasema maneno hayo mara tatu.!!
Harith alisimama huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa ayasemayo Muhammad ni ya kweli, basi tuletee mawe toka mbinguni au utuletee adhabu kali".
Msimulizi wa kisa hiki anasema: "Wallahi hakumfikia ngamia wake bali Mwenyezi Mungu alimpiga kwa jiwe toka mbinguni likaangukia kichwani na kutokea kwenye makalio, akafa. Pale pale Mwenyezi Mungu akateremsha aya hii isemayo:-
 "Muombaji aliomba adhabu itakayotokea (adhabu ambayo) haina wa kuizuia kwa makafiri."
Tukio hili wameliandika wanachuoni wengi wa Kisunni  wasiokuwa wale tuliokwisha kuwataja, basi mwenye kutaka ziyada kutoka katika rejea ni juu yake kutazama kitabu kiitwacho Al-Ghadir cha Al-Allamah Al-Amin.
REJEA
[1] Maarij, aya 1-2
[2] Ibnu Qutaibah, ndani ya kitabu kiitwacho Al-Maarif uk. 251

[3] Imam Ahmad bin Hambal ndani ya Musnad yake Juz. 1 uk.119 

Comments