KWANINI SHIA WANASWALI DHUHURI KISHA LAASIR KATIKA SWALA ZAO

Imeandikwa katika vitabu vya hadithi vya Kisunni kwamba Mtume alizoea kuswali Swala zake kwa kuzitenganisha na halikadhalika kwa kuzichanganya akiwa nyumbani na bila kikwazo chochote. Hadithi nyingi zinathibitisha ukweli huu. Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, katika mlango wa “Jam’a Baina’s-Salatain fi’l-Hadhar,” anasema kwamba Ibn Abbas alisema: “Mtume alizoea kuswali Swala ya Dhuhr na Alasir kwa kuziunganisha na halikadhalika hivyo hivyo kwa Swala za Magharib na Isha bila ya kuwa na kikwazo cha kufanya hivyo, au wakati alipokuwa nyumbani.”

Tena Ibn Abbas alisimulia: “Tuliswali rakaa nane za Dhuhr na Alasir na baadaye rakaa saba za Magharib na Isha kwa kuziunganisha tukiwa pamoja na Mtume.”
Hadithi hiyo hiyo imesimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hambal katika Musnad yake jalada la kwanza, ukurasa wa 221. Halikadhalika, Imamu Muslim ananukuu idadi ya hadithi kuhusiana na suala hili. Anamnukuu Abdullah Bin Shaqiq akiwa amesema kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas alikuwa anahutubia baada ya Swala ya Alasir mpaka jua likazama na nyota zikawa zinaonekana. Watu wakapiga makelele, “Swala, Swala,” lakini Ibn Abbas hakuwajali. Kisha mtu mmoja wa Bani Tamimi alipiga kelele, “Swala, Swala.” Ibn Abbas akasema: “Unanikumbusha mimi kuhusu Sunna, lakini mimi mwenyewe nimemuona Mtume akikusanya Swala za Dhuhr na Alasir halikadhalika Magharib na Isha.” Abdullah Bin Shaqiq
alisema alikuwa hana hakika kuhusu maneno haya na alikwenda kwa Abu Huraira kumuuliza kuhusu maneno hayo. Alithibitisha kile alichokisema Ibn Abbas.
Kupitia sanad nyingine ya wasimuliaji, Abdullah Bin Shaqiq alisimulia kutoka kwa Aqil kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas aliwahutubia watu juu ya mimbari. Alibaki pale kwa muda mrefu mpaka giza likaingia. Wakati mtu mmoja alipopiga kelele mara tatu, “Swala, Swala, Swala,” Abdullah Ibn Abbas alikasirika na akasema: “Ulaaniwe wewe. Unathubutu kunikumbusha mimi kuhusu Swala, ingawaje wakati wa Mtukufu Mtume tulizoea kukusanya Swala za Adhuhr na Alasir na halikadhalika Magharib pamoja na Isha.”

Zarqani katika Sharhe Mawatta cha Imamu Malik, jalada la 1, katika sura ya Jama’a Baina’s-Salatain, ukurasa wa 263, anaeleza, “Nisa’i alisimulia kutoka kwa Amru Bin Haram kutoka kwa Abi Sha’atha kwamba Ibn Abbas aliswali Dhuhr na Alasir na halikadhalika Magharib na Isha kwa pamoja mjini Basra bila kukawia au kitendo chochote kati yao. Alisema kwamba
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali katika njia hii hii.”

Vile vile Muslim katika Sahih yake na Malik katika Mawatta, sura ya Jam’a Baina’s- Salatain, na Imamu Hambal katika Musnad wanamnukuu Ibn Abbas kutoka kwa Sa’id Bin Jabir kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali Swala zake za Dhuhr na Alasir pamoja mjini Madina bila kulazimishwa kufanya hivyo kwa hofu au hali mbaya ya hewa. Abu Zubair akasema alimuuliza Abu Sa’id kwa nini Mtume alikusanya Swala hizo mbili. Sa’id akasema yeye vile vile alimuuliza Ibn Abbas swali kama hilo hilo. Ibn Abbas alijibu kwamba alikusanya Swala hizo mbili ili kwamba wafuasi wake wasije wakawekwa katika uzito na shida zisizo na sababu.

Vile vile, katika hadithi nyingine nyingi,
Ibn Abbas inasimuliwa kwamba alisema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu alikusanya Swala za Dhur na Alasir halikadhalika na Magharib na Isha bila kulazimishwa kufanya hivyo.


Kwa sababu hii hakuna ulazima wa waislamu kuacha shughuli zao mara kwa mara na kwenda msikiti kuswali bali wameruhusiwa kwenda msitini kuswali mara tatu kwa siku ni hivi ndivyo Qur’an inavyosema, ya kuwa nyakati za swala ni tatu japokuwa swala ni tano. Jua linageuka mchana, jua linapozama na subhi basi. Wale wachapakazi ungana na sisi Mashia katika utekelezaji wa ibada kikazi kazi na kuwahi kazi zetu mara moja. Hata hivyo mida wanayoswali masuni haina makosa kwa sababu ni ndani ya mida ya kisheria. 

Comments