MADHARA YA UWAHHABI
Afrika ya Mashariki
imefaidi mazingira ya amani sana kiasi cha karne mbili zilizopita. Watu wa
imani na itikadi zote waliishi pamoja kwa upendo na mapenzi. Kila mmoja
akishiriki kwenye shughuli za mwenzake za kijamii na za Kidini. Ukiangalia
kwenye Jumuiya za Kiislamu, wote wakihudhuria kwenye Misikiti ya kila mmoja,
waliungana pamoja katika Maulidi na hafla za Muharram, na kupanua ushirikiano
wao katika miradi ya kila mmoja. Kama Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi
alivyosema katika hotuba moja ya hadhara;"Misikiti mingi ya Waislamu wa
(Madhehebu ya) Shafi'i iliyoko Zanzibar na Pemba ilijengwa na kutolewa na Shia
Ithna-ashariyya"
Hatimaye
Wahhabi walianza Tabligh (Mahubiri) yao hapa. Badala ya kujaribu kuwaleta
mapagani au wasio waislamu kwenye boma ya Uislamu, nia yao kabisa ilikuwa na
bado inakaziwa katika kuwabadilisha Mashafii wawe Mawahabi. Kwa lengo hili,
hujifanya kama wao ni Masunni, na kuchanganyika pamoja na Masunni.
Mawahabi
hao wamepanda mbegu ya fitina na
chuki kati ya Madhehebu mbali mbali za Kiislamu, na hususan kati ya Sunni na
Shia. Wanazungumza dhidi ya Shia, na kusambaza vitabu na vijitabu (vya mambo ya
dini) dhidi ya itikadi ya Shia ambavyo vimejaa mambo ya uwongo na uzushi.
Kishawishi chao kiko wazi, kwa kuwatenganisha Masunni na Mashia, wakitumaini
kupata urahisi wa kuingia katika jamii ya Sunni na Misikiti yao, ingawaje
tumaini hili lingali bado kukamilishwa katika Tanzania.
Hebu
tuangalie katika mzizi wa uovu wa kampeni hii. Huenda hapo nyuma katika mwaka
1979, ambapo Mapinduzi ya Ki-Islamu yalipotokea katika (nchi ya) Iran, na
watawala wa Kiwahaabi wa Saudia walihadharishwa vikali mno, hata kabla ya tukio
la Mapinduzi ya Kiislamu, wakati Ayatullah al-'uzma al-Khomeini akiwa bado
Najaf (Iraq). Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia, akizungumza
katika hadhara moja ya Waarabu, aliuonya ulimwengu wa Waarabu kwamba kama
Khomeini ataruhusiwa kuendeleza harakati zake kutoka Iraq kama hapo nyuma, sio
tu kwamba utawala wa Shaha utaangushwa, lakini, hali katika eneo lote vile vile
itakuwa imetibuliwa.
Hivyo
wakaishinikiza Iraq kuweka vikwazo juu ya Khomeini kwa hofu ya kwamba, kama
juhudi zake zitafanikiwa katika Iran, zitatingisha tawala zao wenyewe zisizo
imara.
Haikushangaza
kwamba mara tu Mapinduzi ya Kiislamu yalipoimarika nchini Iran, hawa Wahhabi
wakaanza propoganda kali yenye chuki dhidi ya Khomeini, dhidi ya Iran na dhidi
ya Ushia. Kalamu za kukodishwa zikaanza mchakato kutoa vitabu, makala na
vijitabu dhidi ya Shia. Shia waliitwa Makafiri,na
pengine mtu angeuliza: Kama ni Makafiri, basi kwa nini wanapewa viza kwa ajili
ya Hija na Umra? Wairani waliitwa Majus (Waabudu Moto) kwa nini? Kwa sababu
kabla ya kuja kwa Uislamu waliabudu moto. Kwa hoja hii nasi hatuna haki ya
kuwaita Wahhabi Mushrikuna? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu watu wa Najd
walikuwa wakiabudu Masanamu.
Baadhi
ya waajiriwa wao wa ngazi za juu walikuwa ni Ihsan Ilahi Zaheer wa Pakistan, na
Manzoor Ahmad Nu'mani na Abul Hasan Ali Nadwi wa India. Sauti itokayo kwenye
vinywa vyao ni katika watakiwayo na mabwana zao kuyasema, na jambia la uzayuni
lilichovywa kwenye damu ya waislamu linatumika kama kalamu yao. Kitabu
kinachoandikwa dhidi ya Shia na watumwa hawa, kwa miezi michache tu
kinatarujumiwa katika lugha zote kubwa za ulimwengu wa Kiislamu; na hufanywa
kipatikane kila mahali, kadhalika husambazwa bure miongoni mwa Mahujaji:
Kwa
msingi huu ninasema kuwa Mawahhabi ni mushirikina wenye kuabudu Masanamu. Kutokana
na imani hii potofu ndio maana utawasikia wakisema Allah (s.w) ana viungo kama
binadamu, yaani macho, masikio,miguu na pia husafiri toka sehemu moja hadi
nyingine.
Comments
Post a Comment