Allah (s.w) anasema, "Enyi waumini, mkimcha Mwenyezi Mungu atakuongozeni
njia ya haki na atawafutieni makosa yenu na atakusameheni". (8:29).
Uchamungu ni
moja ya pambo lenye thamani kwa binadamu na ni kipimo cha haki na batili na
kila ambacho kinamfanya mwanadamu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kwani
uchamungu ni vazi zuri lenye thamani kwa kila ataelivaa, hupata ukunjufu wa
moyo na hima ya kutafuta haki hadi kufikia kikomo na kuwa karibu na Mwenyezi
Mungu, neema zake, zikitiririka bila ya hesabu.
Katika
ulimwengu huu ambao umejaa ibilisi wenye rangi tofauti, wakiwa na mitego
tofauti ili kuwanasa wanadamu kwa vishawishi vipotovu na kuwatoa katika misingi
ya haki na ya ukweli na yenye mwelekeo wa tawhid. Wale ambao waliofahamu hila
za ibilisi na wakakana kudhalilishwa kwa kufuata vishawishi vyake, kwa hakika
hawa ni katika waongofu.
Jambo lakusikitisha, kwamba kwa upande mwingine makafiri wana hila zao, nara zao zaweza kuonekana kuwa ni uchamungu na wakafanya vitendo viovu wakiona ni vya kumridhisha Mwenyezi Mungu, hali ya kughafilika kwamba huo ni upotovu na ni chanzo cha kuangamia, lakini Mwenyezi Mungu amewaahidi wale wamchae kuwaonyesha njia ya haki.

Mfano wa
hawa waovu ni wakristo ambao wamemfanya Yesu mwana wa Mariam kuwa Mungu badala
ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na kutumia nguvu nyingi kumtangaza kuwa ni Mungu
kiasi kwamba unaweza kushindwa kujua kuwa ni watu waliopotoka.
Wengine na
Mawahhabi, Answari Sunah na Masalafi ambao ni watu wenye hasira kali, ni wepesi
wa kulipiza kisasi na hawasiti kumuua yeyote watakaye amua kumuua. Yote haya ni
makundi ya ibilisi yanayojificha kwenye dini. Tujiepushe nayo na kimbilio letu
ni Uislamu sahihi kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlulbayt wake (a.s).
Comments
Post a Comment