MAONI YA BAADHI YA MASAHABA KUHUSU WENZAO JINSI WALIVYOBADILI SUNNAH ZA MTUME

Imesimuliwa toka kwa Said Al-Khudri kuwa Mtume alikuwa akitoka siku ya Idil Alfitri na Adh-ha kwenda kuswali, basi alikuwa akianza na swala kisha khutuba. Lakini amiri wa Madina Marwan alikuwa akianza khutuba kisha anamalizia kwa swala ya iid. Alimwambia Marwan mmebadilisha, akasema, ewe Baba Saidi yamekwisha ondoka uyajuayo. Kwa hakika watu walikuwa hawakai nasi baada ya kuswali ndipo tumefanya khutuba kabla ya swala.
(Tazama: Sahihi Bukhari Juz. 1 uk. 122).
Ukweli ni kuwa watu waliacha kusikiliza hotuba za watawala wa kipindi hicho kwa sababu ya khotuba zao zilizokuwa zimejaa matusi dhidi ya Ahlulbayt wa Mtume na hasa dhidi ya Imam Ally (a.s). Hii ilitokana na watawala waovu wa Bani Umayyah wakiongozwa na Muawiyyah bin Abi Sufian ambaye aliagiza Imam Ally atukanwe kwenye mimbari ili kuufuta utukufu wa Ahlulbayt wa Mtume. Sahaba Hujru ibn Adiyi na ndugu zake walizikwa wakiwa hai kutokana na kupinga agizo hilo haramu la Muawiyyah.
(Tazama sahihi Muslim, mlango wa Fadhail za Ali ibn Abi Talib)
Naye Abul-ala Al- Maudud ameandika ndani ya kitabu chake kiitwacho Al-Khilafahtu wal-Muluku (uk. 106), akimnukuu Al-Hassan Albasri kuwa:
Mambo manne alikuwa nayo Muawiyah, lau asingekuwa nayo isipokuwa moja tu bali lingetosha kumwangamiza. Mambo hayo ni:
1. Kuchukua ukhalifa bila ushauri wakati walikuwepo Masahaba bora kuliko yeye,
2. Kumrithisha ukhalifa mwanawe (Yazid) aliyekuwa mlevi, anayevaa Hariri na kupiga zumari.
3. Kumfanya Ziyad kuwa mwanawe wakati Mtume amesema, Mtoto ni wa kitanda na mzinifu wa kiume atapata jiwe.
4. Kumuua Hujru bin Adiyi na ndugu zake. Basi ole wake kwa kumuua Hujru bin Adiyi na jamaa zake
Masahaba hawa walibadili na kugeuza na wakasema tumesikia na tumeasi. Badala ya kumuombea rehema Imam Ally, kumpenda na kumtii, wao walimtukana na kumlaani kwa muda wa miaka 60 kama ilivyoelezwa ndani ya vitabu vya Historia.
Basi kama watu wa Mussa (a.s) walivyofanya njama dhidi ya Harun (a.s) na wakakaribia kumuua. Hakika baadhi ya Masahaba wa Mohammad (S.A.W.W) walimuuwa Harun wake (Imam Ally) na wakawafuatilia watu wake na wafuasi wake kila upande wa dunia, wakayafuta majina yao katika diwani na wakazuwia mtu yeyote asiitwe kwa jina lake. Haikutosha hiyo bali waliwalazimisha Masahaba wengine waungane nao katika dhuluma hiyo dhidi ya aali Mohammad (a.s).
Mtume anasema nini kuhusu Imam Ally (a.s):
1. Ally anatokana nami na mimi ninatokana naye
2. Kumpenda Ali ni dalili ya Imani na kumbughudhi ni dalili ya unafiki
3. Mtume ni jiji la elimu na Ally ni lango lake
4. Ally ni walii wa kila muumini baada yake
5. Ali ni wasii na khalifa wa Mtume baada yake
Rejea: Musnad Ahmad juz. 5 uk. 25

Comments