MAONI YA MTUME MOHAMMAD (S.A.W) KUHUSU MASAHABA WAKE

Mtume amesema, “Nitakuwa nimesimama (siku ya Qiyama) halafu watanijia watu, na nitakapowafahamu, atatokea mtu kati yangu na wao atasema, (kuwaambia) twendeni, mimi nitasema waende wapi? Atasema motoni, nitasema wemefanya nini hawa? Atasema, hakika wao walirudi kinyume nyume baada yako. Basi sitowaona wenye kuokoka miongoni wao isipokuwa kikundi kidogo”.
Na amesema Mtume, “mimi ni mtangulizi wenu kwenye hodhi, yeyote atakayepitia kwangu atakunywa na atakayekunywa hatosikia kiu milele, bila shaka watanifikia watu mbali mbali ambao mimi ninawafahamu na wao wananifahamu, kisha patawekwa kizuizi baina yangu na wao, mimi nitasema, hao ni masahaba wangu, patasemwa, hakika wewe hujui mambo waliyoyazusha baada yako, basi mimi nitasema, aangamie aliyebadilisha dini yangu.”
Rejea;
1. Sahihi Bukhari Juzuu 4 uk. 94, 99, 156
2. Sahihi Bukhari Juzuu 3 uk. 32
3. Sahihi Muslim Juzuu 7 uk. 66 Hadith ya Haudh
Yeyote atakayefanya mazingatio katika hadith hizi mbili zilizoandikwa na wanazuoni wakubwa kabisa wa kisunni atagundua kuwa wengi wa Masahaba walibadilisha dini na kurtadi muda mfupi tu baaada ya Mtume kufariki dunia. Hili sio kundi la wanafiki kwani Mtume amesema Masahaba wangu kwa maana kuwa hadi Mtume anafariki wao walikuwa ni Masahaba kisha wakauacha Uislamu sahihi na kugombea madaraka na hivyo kuiacha serikali sahihi ya Kiislamu. Tunaweza kuthubutu kusema kuwa Khilafah sahihi iliondoka siku Mtume alipokufa. Tawala zilizofuatia zilitokana na tamaa za madaraka za waheshimiwa kama Abubakar na Umar. Kwa kuwa baada ya Mtume kufa hakuna tukio kubwa lililotokea isipokuwa uporaji wa utawala toka kwa Ahlulbayt wakiongozwa na Imam Ally na Fatumah bint Rasulillah na madaraka hayo yakanyakuliwa na mabwana wakubwa Abubakar bin Quhafah na Umar bin Khatab. Watu hawa wawili waliongoza kikao haramu cha mapinduzi kipindi ambacho waislamu sahihi walikuwa wakimzika Mtume. Na kwa kuwa waislamu waliowengi hawakukemea dhuluma hiyo bila shaka kurtadi alikokusudia Mtume ni kupindua serikali aliyoiacha chini ya Imam Ally.

Comments