MATENDO MAOVU YA UKHALIFA WA BANI UMAYYAH (VIONGOZI WA MAWAHHABI)

Kwa desturi viongozi wa bani Umaya walikuwa wakiwawamba msalabani watu waliowaona kuwa ni wapinzani wao. Na hata akifa mpinzani walikuwa wakiifukua maiti yake na kuitundika na kusambukia msalabani.
Kwa kuzingatia maovu ya ufalme huu uliolaaniwa, mwili wa Amiru’l-Muminin, ‘Ali (as) ulizikwa wakati wa usiku, na hakuna alama ya kaburi hilo iliyoachwa. Kaburi likabakia bila kuonekana mpaka wakati wa Khalifa Harun ar-Rashid. Siku moja Harun alikwenda kuwinda katika eneo la Najaf, ambako paa waliishi kwa wingi.
Wakati mbwa walipofukuza paa, walichukua hifadhi juu ya kilima kidogo (kilichotutumka juu ya ardhi) cha Najaf, kilima ambacho mbwa hao hawakuweza kukipanda.
Mara nyingi wakati mbwa waliporudi nyuma, paa waliteremka chini, lakini wakati mbwa wanapowarukia tena, wale paa huchukua tena hifadhi juu ya kile kilima.
Harun akatuma watu wake kwenda Najaf kuuliza. Walimleta mzee mmoja kwake na Khalifa akauliza kuhusu siri ya kwa nini mbwa hawakupanda juu kilima.
Kugunduliwa Kwa Kaburi Tukufu La Ali.
Yule Mzee akajibu kwamba anaielewa Siri yake, lakini alikuwa anaogopa kuitoa. Khalifa akamhakikishia usalama wake, na yule mzee akamwambia: Siku moja nilikuja hapa pamoja na baba yangu, ambaye alipanda juu ya kilima na akaswali pale.

Nilipomwuuliza kuna nini pale, akasema kwamba waliwahi kuja pale na Imam Ja’far Sadiq kwa ajili ya Ziara. Imam alisema kwamba hili ni kaburi Tukufu la Mheshimiwa babu yake, Amur’l Mu’miniina Ali, na kwamba muda mfupi litakujajulikana.”

Kwa amri ya Khalifa sehemu ile ilichimbuliwa, na alama za kaburi zikaonekana wazi pamoja na ubao wenye maandishi ya Ki-Syria yenye maana; “Kwa jina la Allah, Mwenye rehema, Mwenye kurehemu. Kaburi hili limetayarishwa na Mtume Nuh kwa ajili ya Ali, wasii wa Muhammad miaka 700 kabla ya gharika.”

Khalifa Harun alitoa heshima zake kwenye sehemu ile na akaamuru ule udongo urudishwe. Kisha akasali rakaa mbili. Alilia sana na akajilaza juu ya kaburi. Baadae, kwa amri yake, taarifa ya tukio lote ilitolewa kwa Imam Musa Kadhim huko Madina. Imam alithibitisha kwamba kaburi hilo ni la Mheshimiwa babu yake, Amiru’l-Mu’minin Ali, lipo mahala hapo.

Kisha Harun akaamuru jengo la mawe lijengwe juu ya kaburi tukufu la Amiru’l-Mu’minin, ambalo lilikuja kujulikana kama “Hajar Harun.” Kwa wakati huo habari zilisambaa na Waislamu wakaizuru sehemu hiyo tukufu.
Huu ni ushahidi kuwa Bani Umaya na mawahhabi wanapinga uongozi wa Imam Ally (a.s) kwa sababu ya tamaa na hiyana, lakini nafsi zinawasuta kuwa hakuwahi kuwepo Mtu bora Kama Imam Ally, baada ya Mtume (s.a.w.w). Kama isingekuwa hivyo kwanini akalijengee kaburi la Imam Ally badala ya Mawiyyah au Uthuman?

Lakini vile vile wanaopinga kujengea makuburi wamezua bida’a ambayo hata viongozi wao wakifufuka watawashangaa.


Na mwisho kuswali maeneo yenye makaburi sio kuyaabudu kama wanavyodanganya mawahhabi na masalafi vinginevyo wakubali kuwa hata viongozi wao walikuwa washirikina. 

Comments