MATENDO YA MWEZI MTUKUFU WA SHAABAN NI HAYA YAFUATAYO:

1-FUNGA:
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): (Mwenye kufunga siku ya Jumatatu na Alkhamisi ya mwezi wa Shaaban, Mwenyezi Mungu mtukufu atamuwekea fungu lake, na mwenye kufunga siku ya Jumatatu na Al-khamisi ya mwezi wa Shaaban atakidhiwa haja ishirini katika haja za kidunia, na haja ishirini kati ya haja za Akhera [6].

Na imepokelewa kutoka kwa Amiril-muuminiin Ally (a.s) ya kuwa amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): (Kila Al-khamisi ya mwezi wa Shaaban mbingu hupambika, na malaika husema ewe Mola wetu msamehe mfungaji wa mwezi huu, na wajibu dua zao (hadi akafikia kusema) na mwenye kufunga kwenye mwezi huu siku moja Mwenyezi Mungu huuharamisha mwili wake kuingia Motoni) [7].

Na amesema kiongozi wetu Amiril-muminiin Ally (a.s): (Mwenye kufunga mwezi wa Shaaban kutokana na mapenzi yake kwa Mtume (s.a.w.w) na kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu alie takasika basi Mwenyezi Mungu atampenda na kumkaribisha kwenye ukarimu wake siku ya kiama na atamuwajibishia pepo ) [9].

Na Imamu wetu Abu Jaafar Al-baaqir (a.s) akasema: (Hakika funga ya mwezi wa Shaaban ni funga ya manabii, na ni funga ya wafuasi wa mitume, basi mwenye kufunga mwezi wa shaaban kwa hakika atakuwa amefikiwa na wito wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kutokana na kauli yake, Mwenyezi Mungu amrehemu mwenye kunisaidia juu ya mwezi wangu huu) [10].
Na Abu Abdillahi As-swadiq (a.s) akasema: (Mwenye kufunga siku moja ya mwezi wa Shaaban ataingia peponi) na (Mwenye kufunga siku tatu katika mwezi wa Shaaban atawajibikiwa na pepo, na Mtume (s.a.w.w) atakuwa muombezi wake siku ya kiama) [11].
Na imekuja kutoka kwa Hasan bin Ali bin Shuubah Al-harraniy katika kitabu chake (Tuhaful-ukuul) kutoka kwa (Imam Ridhaa (a.s) katika barua yake kuelekea kwa Maamun amesema: (Na funga ya mwezi wa Shaaban ni jambo njema nayo ni sunna) ([12]).


2- KUFANYA ISTIGHFARI
Hilo litatimia kwa kusema kila siku mara sabini: (Astaghfiru llah wa’as’aluhut-tawbah) na (Astaghfirullah alladhi laa ilaha illa huwar-rahmanir-rahiim, al-hayyil-qayyum wa atuubu ilaihi).
Na tunafaidika kutoka kwenye habari hii kuwa dua  na nyuradi zilizo kuwa bora zaidi katika mwezi huu mtukufu ni kuomba istighfari.
Amesema Imamu Ridhaa (a.s): (Mwenye kumuomba Mwenyezi Mungu istighfari katika mwezi wa Shaaban mara sabini, Mwenyezi Maungu atamsamehe madhambi yake, hata kama yatakuwa ni kiasi cha idadi ya nyota) [13].


3- KUTOA SADAKA
Kiasi kiwezekacho hata kama ni kipande cha tende.
Aliulizwa Imam Swaadiq (a.s): Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! ni tendo gani bora kati ya matendo yafanywayo katika mwezi wa Shaaban? Akasema: (Ni kutoa sadaka na kufanya istighfari, na mwenye kutoa sadaka katika mwezi wa Shaaban Mwenyezi Mungu mtukufu atailea kama ambavyo mmoja wenu aleavyo mtoto wake hadi aweze kulipwa siku ya kiama na imekua kubwa na kuwa kama mlima wa Uhud) [14].

4-KUSOMA TAHLIIL (YAANI: LAA ILAHA ILLA LLAH)
Na atafanya tahliil katika siku zote za mwezi mara elfu moja:

(لا إله إلا الله ولا نعبد إلا إيّاه مخلصين له الدين ولو كره المشركون)   
5-KUSALI RAKAA MBILI
Kila siku ya Al-khamisi ya mwezi mtukufu wa Shaaban.
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): (Mwenye kusali rakaa mbili katika mwezi huu: akisoma katika kila rakaa Suuratul-fatiha na Qul-huwallahu ahad) mara mia moja na akitoa na kumsalimia Mtume (s.a.w.w) mara mia moja Mwenyezi mungu atamkidhia haja zake zote kati ya mambo yake ya dini yake na  dunia) [15].

6-KUSOMA SWALAWAAT ILIYO POKELEWA KUTOKA KWA IMAMU WETU ZAINUL-ABIDIIN (A.S)
Kila mchana kati ya siku za mwezi wa Shaaban na katika usiku wa nusu ya mwezi huo na swalawat hiyo ni hii ifuatayo:

(بسم الله الرحمن الرحيم، اللهم صلّ على محمد وآل محمد شجرة النبوة وموضع الرسالة ومختلف الملائكة ومعدن العلم وأهل بيت الوحي و...).


7-KUSOMA MUNAAJAATI ULIO POKELEWA KUTOKA KWA AMIRIL-MUUMINIIN (A.S)

Na ulio maarufu kwa jina la (Al-munajaatish-shaabaniyyah na matni yake imo kwenye vitabu vya dua.
[1]-Al-aamal cha Swaduuq.
[2] -Mustadraku wasaailu shia\ Juzu 7 \ Abwaabu swaumul-mandub \ Babu Istihbabul-istighfar wa…..fii shaaban\ ukurasa 544\ chapa ya Muassasah Aalul-baiti liihyaait-turaath\ chapa ya kwanza 1407 hijiria.
[3] -Al-amaal cha Swaduuq.
[4] -Tafsiri Majmaul-bayaan ya Twabarasiy juzu\ 5.
[5]-Mustadraku wasaailu shia juzu \ 7 chapa ya Muassasatu Aalul-baiti li’ihyaai turaath, Abwaabus-swaumu al-manduub\ baabu istihbaabul-istighfari wa… fii shaaban \ukurasa 542.
[6] -Wasaailu shia \ kitaabus-swaumu \ Abuwaabus-swaumul-manduub \ Istihbaabu swaumu shaaban\ ukurasa 366 \ Daru ihyaau turaathil-arabiy \chapa ya nne 1219 hijira.
[7]-Chanzo kilicho tangulia.
[8]- Chanzo kilicho tangulia.
[9]-Chanzo hichohicho.
[10]-Chanzo kilicho tangulia.
[11]-Chanzo kilicho tangulia.
[12]-Tuhaful-ukuul \ baabu kalimaatul-imam Ridhaa (a.s).
[13]-Mustadraku Safiinatul-buhaar \ cha Namaaziy – juzu 5 \ 414.
[14]-Iqbalul-aamal cha Sayyid ibnu Twaawus \juzu 3 \ 294.

[15]-Wasailu shia \ chapa ya Aalul baiti \ juzu 8 \ 104.

Comments