Siku moja wakati wa darasa mwalimu Yusuf aliwauliza wanafunzi wapendwa, “je vitu gani vinavyo Linda miti mikubwa na imara dhidi ya upepo mvua za mafuliko”. “miti mikubwa na imara hulindwa na mashina” mmoja wa wanafunzi alijibu kisha mwalimu aliuliza, “mashina ya miti hulindwa na vitu gani?” Ahmad mwanafunzi mahiri na hodari, mwenye bidii, alijibu hivi, “mizizi hulinda mashina” mwalimu alisema “vizuri sana” kisha aliongeza, kama ilivyo baadhi ya miti ina mizizi chini ya ardhi na ile tuionayo juu ya ardhi, mizizi hii hulinda miti iliyo simama kwa kipindi cha muda mrefu dhidi ya mabadiriko mbalimbali. Hivyo, pia dini ya Uislamu ina mizizi inayolinda mti wa Uislamu. hii huitwa mizizi ya Uislam. Bila hiyo Uislam usingeliishi au kuwepo.
Baadaye mwalimu Yusuf aliuliza swali lingine, “je kuna miongoni mwenu anaye fahamu mizizi ya dini ya kiislam ambayo imeleta uthabiti wa mti wa Uislam.” Uthuman alinyoosha mkono na alijibu hivi. “Mizizi ya Uislam ni mitatu ambayo ni upweke wa Allah [SW] at tawhid, utume au unabii [an nubuwah] na ufufuo [al maad]. vizuli sana mwalimu alisimama kisha alianza kuielezea zaidi mizizi hii mitatu hivi. upweke wa Allah [SW] ni kumuamini Allah [SW] na umoja wake na ni yeye pekee aliye umba na kuingoza dunia. ama kwa unabii au utume ni kuamini kuwa Allah [SW] amewatuma manabii ili kuwaongoza wanadamu. kuhusu ufufuo ni kuamini siku ambayo watu wote watafufuliwa baada ya kufa ili kulipwa matendo yao wachamungu wataingizwa peponi na waovu wataingizwa motoni
Mwalimu Yusufu pia aliwauliza wanafunzi kwa nini ninyi ni waislamu? “Kwa sababu babu, baba na mama ni waislam, nasi pia ni waislamu”. alijibu Ibrahim. mwalimu Yusufu alisema kila mmoja analazimika kukubali au kupokea mizizi ya dini ya kiislamu ambayo ipo katika nguzo tatu kwa misingi ya ushahidi tu. Kwa hivyo lazima tufahamu kwamba Allah [SW] yupo kwani ametuma manabii kwa ajili ya uongozi wa mwanadamu.
Mwisho wa somo mwalimu Yusufu alisema, “sifa muhimu sana zaidi ni kuwa lazima sisi tukubali mizizi ya Uislam kwa misingi ya ushahidi na hatuwezi kusema kuwa tumekuwa waislamu kwa kufuata baba na mama zetu ambao walikuwa ni wa waislamu.
Somo lilifikia mwisho na wanafunzi wote waliridhika na sehemu za habari mpya walizo jifunza.
Mwisho wa somo mwalimu Yusufu alisema, “sifa muhimu sana zaidi ni kuwa lazima sisi tukubali mizizi ya Uislam kwa misingi ya ushahidi na hatuwezi kusema kuwa tumekuwa waislamu kwa kufuata baba na mama zetu ambao walikuwa ni wa waislamu.
Somo lilifikia mwisho na wanafunzi wote waliridhika na sehemu za habari mpya walizo jifunza.
Comments
Post a Comment