MTUME AMTANGAZA IMAM ALI KUWA KHALIFA WAKE

Iliposhuka aya 26:214 Mtume aliwaambia jamaa zake, “Enyi Bani Abdul Muttalib! Hakika mimi wallahi simjui kijana yeyote katika waarabu, aliyewaletea watu wake jambo bora kabisa kuliko nililokuleteeni mimi. Hakika mimi nimekuleteeni kheri ya dunia na akhera na ameniamrisha Allah nikuiteni kwake, basi ni nani kati yenu atanisaidia jambo hili ili awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu?”
Watu wote wakanyamaza, nikasema (Ali), “mimi ewe nabii wa Allah! Nitakuwa waziri wako, Pale pale Mtume akanishika shingo yangu, kisha akasema, ‘hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu, kwa hiyo msikilizeni na mtiini.’”
Kwa hiyo Ali bin Abi Talib, ni wasii na khalifa wa Mtume (S.A.W.W) kwa waislamu. Wasii ni mtu anayesimama kuendesha mambo ya mtu. Kwa kuwa Ali ni wasii wa Mtume, maana yake Ali atasimamia na kuendesha mambo ya waislamu baada ya Mtume.
Khalifa ni mtu anayekuja kukaa mahala pa mtu mwingine baada yake. Kwa kuwa Ali ni khalifa wa Mtume maana yake ni kuwa Ali atashika mahala pa Mtume baada ya Mtume.
TAZAMA:
1. Tarekhut Tabari; Juzu 2 uk. 63
2. Tarekh Ibn Athir; Juzu 2 uk. 62 -63
3. Tafsirul Khazin; Juzu 5 uk. 127
4. Assiratul Halabiyya; Juzu 1 uk. 311
5. Sabilun Najaati: uk. 113

Comments