MUANDAMO WA MWEZI

Mwezi wa Ramadhani unakaribia, waislamu tutaanza kushutumiana kuhusu mwandamo wa mwezi. Kuna watu wanasema kuwa mwezi ukiandama popote duniani tufunge, lakini cha kushangaza ni kuwa wao wanaangalia mwezi unaoandama Saudi Arabia tu na wala sio nchi zingine. Najiuliza hizi ni siasa au dini? Mwaka jana kuna nchi mbili za Afrika Magharibi, mwezi uliandama kabla ya Saudi Arabia lakini hawakufunga, japokuwa taarifa ziliwafikia walizipinga na wakaendelea kuongoja Saudi Arabia watangaze. Kama kweli ni utaratibu kufuata mwezi unaoandama popote duniani, Saudi Arabia nao wafuate mwezi unaoandama huku kwetu. Kwa ukweli watetezi wa hoja hii ni wale wanaopata mshahara kutoka serikali ya Saudi Arabia na huu ni aina Fulani ya ukoloni.
Waislamu tuliowengi tunafuata hadith ifuatayo inayotuelekeza kila eneo liangalie mwezi unaoandama katika eneo lao.  Ibn 'Abbaas anamnukuu Kuraybu, "Ummul Fadhli bint Harith [mama yake Ibn 'Abbaas] alinituma kwa Muawiyya katika mji wa Shamu nikafika Shamu na kutekeleza haja zake [zote] na ukaonekana mwezisayari wa mwezi wa Ramadhaan, na mimi nipo Shamu, tukauona mwezisayari usiku wa kuamkiya Ijumaa, baada ya hapo nikarudi Madina mwisho wa mwezi [wa Ramadhaan] akaniuliza Ibn 'Abbaas, kisha akautaja mwezi akasema: lini mliuona mwezi? nikamwambia usiku wa kuamkiya Ijumaa. Akasema kuniuliza wewe umeuona usiku wa kuamkiya Ijumaa? Nikajibu ndiyo na wameuona watu [wote] na wakafunga, na akafunga Muawiyya [piya] akasema Ibn 'Abbaas lakini sisi tumeuona mwezi usiku wa kuamkiya Jumamosi na tutaendeleya kufunga mpaka tukamilishe siku 30, au tuuone[wenyewe], nikamwambiya [Ibn 'Abbaas] je, hukutosheka kwa kuuona Muawiyya na kufunga kwake akajibu kwa kusema, "hivi ndivyo alivyotuamrisha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)."

Sanad ya Hadith hii ni sahihi na haina shaka kwa mfano angalia sanad ya Al-Tirmidhi utaona sanad inasema kwa uwazi: .."Katuhadithia Muhammad bin Abi Harmala katupa habari Kurayb ". Na katika masimulizi ya Abu Daud: ".Katupa habari Muhammad bin Abi Harmala katupa Habari Kurayb". Na katika masimulizi ya Ibn Khuzaima: " Kutoka kwa Muhammad (yaani bin Abi Harmala) kutoka kwa Kurayb". Na katika masimulizi ya Al-Nasaai: " Katuhadithia Muhammad - naye ni Ibn Abi Harmala - kasema kanipa habari Kurayb". Na katika masimulizi ya Al-Bayhaqi: "Kutoka kwa Muhammad bin Abi Harmala kutoka kwa Kuraib".

KUMJADILI KURAYBU

 Watukufu Waislam mpokezi wa hadith hii Kurayb kama ilivyotajwa hapo juu. Labda tutahitaji kumjua kama ni mwenye kuaminika. Kuraybu ni mtu ambaye wanachuwoni wa hadith wanamkubali kuwa alikuwa mtu mkweli sana na anategemewa katika upokezi wa hadithi tazama kitabu 'Tahdhibu' cha Imam Ibn Hajar Al 'Asqalani [jalada la 3 uk 468 chapa ya Beirut tazama mahala pa herufi kaaf] Na tazama vile katika Taqribu Tahdhibu cha huyu huyu Ibn Hajar Al Asqalani jalada la 2, uk 28. 

Comments