Imamun-Nawawy aliyekisherehesha Kitabu cha Sahihi Muslim anasema:
"Na jambo lililo sahihi kwa wenzetu (Mashaffi) ni kuwa muandamo mmoja hauwahusu watu wote bali unawahusu wale walio karibu kwa kiasi ambacho hawaruhusiki kupunguza Sala (Sala ya safari). Pia imesemwa kuwa iwapo matlai ni mamoja watalazimika (watu) kufunga pamoja. Pia imesemwa kuwa ikiwa (wanaishi) katika eneo la Iklimu moja (maili 72 au km 89) (watalazimika kufunga pamoja) vyenginevyo kila mmoja atafunga kwa muandamo wake.

Asemaye kuwa tufunge kwa muandamo mmoja, hoja yake ni Hadithi
"Fungeni kwa kuuona"; na anayesema kuwa kila mahala na muandamo wake,
anatoa ushahidi wake ni Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib. Hapa kuna ijtihad katika
kuyafahamu maandiko haya: Kuona huku kwa mwezi kumekusudiwa kuonekana na
Waislam, na kuonekana na Waislamu huko, sio lazima kuonekana na Waislamu wote.
Bali inatosha shahada ya mtu mmoja muadilifu".
Shaykh Ahmad Al Khalil, Mufti wa Omani amethibitisha kwamba Ikhtilaf hii ya muandamo wa mwezi katika hukmu ya kufunga au kufungua ipo na kwamba ni jambo la kale. Kama alivyosema maneno yake yaliyotafsiriwa na Shaykh Muniir Sulayman 'Aziz kwamba: "Hakuna madhehebu iliyokuwa imesalimika na kuwa na Khitilafu baina ya Wanavyuoni wake juu ya suala la kutafautiana miandamo ya mwezi."
Lakini ukweli ni kuwa hata katika nchi nyengine zote za dunia taqriban kauli kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ni kauli ilioishia katika vitabu tu, kimatendo (practically) kauli hio haitumiwi isipokuwa na mtu mmoja mmoja. Hadi leo hii: watu wa Yemen wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao, Misr wanafata muandamo wao na nchi zote taqriban ni hivyo.
Hili ni suala la khilafu kwa hivyo tusigombane kila mtu afate rai anayoiona kuwa ni sawa.

Comments
Post a Comment